Mwenye uhiitaji wa kuangaliziwa nyumba nipo

Hilo balaa nililiona Mwanza baraza la ardhi yule mhaya sijui alipata wapi document mwenye mali nae anazo zenye jina lake nyumba 1 wamiliki 2 kesi bado inaendelea ila kawa mpole kwa mbinde kaomba apewe kitu kidogo aondoke ila ni muda sasa wanavutana!

Niliombwa na mtu akae kwenye nyumba yangu ipo mkoa flani ila taarifa nilipewa na jirani yangu kuwa kuna mtu anaomba ailinde, aiseeh kumuona anayeiomba akaemo mbingu na ardhi bahati nzuri mi nae mwili sindano kubwa akaomba nimuonyeshe mwenye nyumba nikasema anipe muda. Yaani nyumba haijasakafiwa ni paa na gril tu kitambi kile ukiweke mule kweli? Big No

I never trust anybody kila la kheri mkuu
 
Kazi kwako 👇

Hata picha amekuwekea ushindwe wewe
 
Maisha yako yote kila mtu mfanye adui kwenye mali zako hata kama ni ndugu wa damu, kwa maana ya kuandikishana kwa lawyer na mda wowote ukihitaji mali yako unachukua

Hii story ya hivi ilitokea jijini mzee aliuza nyumba yake kwa mzee mwingine kwa 300m (pagala) kariakoo miaka ya nyuma
Mzee kachukua chake akaomba kwa tajiri aendelee kukaa kwa mda kumbe hela kawagawaia baadhi wanae, akakubaliwa kuishi hapo

Baada ya miaka 3 mzee mwenye eneo akaamua kupiga chini ashushe mjengo waswahili wakamwambia usikubali kuhama mpaka akutoe
Kesi polisi nao wakaona dili wakasema shikilia hapo hapo
Jamaa zilimtoka 30m kumhamisha na kumtoa hapo
Kuna watu wana roho mbaya sana
Hakikisheni mnaandikishana pamoja na kuwa mali ni yako maana wakikaa sana watoto huwa wanasema tumeishi maisha yote hapa ni kama kwetu especially mashamba na huwatoi
 
fact.
 
Shida huko ni mbali na uchumi wangu sio mzuri kwa kuhama mkoa mkuu
 
Umesema kweli watu saivi wamekuwa wana roho za unyama sana hata uliyeishi nae kwa uaminifu bado haitoshi kumwamini hasa vitu kama hivi
 
Dah comments za watu zimenichanganya kuna mama nimemwachia aniangalizie nyumba mabinti zake wanalala pale ila na wao wana nyumba ni majirani na nilipojenga
 
Wasi wasi wa nini?.
Siku unataka nyumba yako unawaambia wahame.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Kabisa nyumba yenyewe nimeshaimaliza imebaki vitu vidogo tu nimeshindwa kuhamia kwasababu nafanya kazi mbali na nilipojenga na sina familia bado
Ningeiacha hivihivi bila mtu ingechakaa maana nyumba nayo inahitaji usafi
 
Umesema kweli watu saivi wamekuwa wana roho za unyama sana hata uliyeishi nae kwa uaminifu bado haitoshi kumwamini hasa vitu kama hivi
Tulikuwa na shamba na jirani akaomba alime kwa kuwa tulikuwa hatulihitaji kwa wakati huo
Tatizo likaja siku alipokufa, wanae wakaweka mipaka wanayojua wao
Yaani kipande kikubwa cha shamba letu wakachukua tukaona isiwe shida ingawa wamekua kwa chakula alicholima baba yao kwa kupitia na shamba letu
Yaani ukiwa na roho ndogo unaweza kuuwa

Mkuu dawa ni kuandikishana na Shahidi wawili hakuna ukaribu wala kujuana kwenye mali
 
Dah comments za watu zimenichanganya kuna mama nimemwachia aniangalizie nyumba mabinti zake wanalala pale ila na wao wana nyumba ni majirani na nilipojenga
Kaza acha uwoga
 
Kabisa nyumba yenyewe nimeshaimaliza imebaki vitu vidogo tu nimeshindwa kuhamia kwasababu nafanya kazi mbali na nilipojenga na sina familia bado
Ningeiacha hivihivi bila mtu ingechakaa maana nyumba nayo inahitaji usafi
mali ya mtu haipotei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…