Mwenye ujuzi wa pikipiki za shineray

Mwenye ujuzi wa pikipiki za shineray

Ndengaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,831
Reaction score
14,259
Nipo kwenye process ya kununua pikipiki na huwa napendelea pikipiki yenye umbo kubwa kiasi, kwa Tanzania hizi shineray ndio zinaonekana cheap, kwa mwenye uzoefu na hizi anijuze, fuel consumption sio tatizo, ningependelea kujua stability price na sehemu ninayoweza kuipata kwa bei nzuri.
 
mmh siku moja road siku mbili kwa fundi kubaliana na mwendo huo
 
Mkuu mm nimtumiaji mkubwa wa pikipiki hizo pikipiki kubwa kama shineray, Toyo na hata T better hazina utafauti sana na zina ubora hafifu sana kuanzia kwenye injini hadi sehemu nyingine za nje pia hazifai kwa mizunguko mingi na zikiwa njiani ni nzito kuchanganya na pia zina mitetemo sana hivyo jiandae kwa magojwa ya mgongo soon achana na mitazamo ya kutumia pikipiki kubwa hasa kama unaishi mjini kuna pikipiki ndogo ambazo utaenjoy kama Honda ace wengi huziita Honda manji, Tvs125 na ukishindwa kabisa go for hero au boxer. Hizo shineray hata kuuzika kwake ni kazi sana pindi zinapomaliza matumizi na pia hazifai kabisa kwa shuruba na ikichoka kdg mlio wake utadhani unawapa lift waganga na manyanga yao kifupi pikipiki kubwa ni nzuri kwa safari moja moja na sio mizunguko mingi nisisahau na kelele wakati wa kuendesha ukitembea km 30 ukifika masikio hayasikii vzr.
 
Tupe maelezo ya kina boss utasaidia sana
injini zake siyo imara yaan kuzingua ni kawaida yake halafu cheses yake inakatika hovyo hata kama hubebeshi mizigo mikubwa yaani adui wa hizo pikipiki ni kwenye barabara za mashimo.
 
Mi natumia yamaha clux mwaka wa tano namwagaga oili tu dah naipenda xana ila bei yake ni sawa na vits
 
Hapo hakuna pikipiki chesis yake inakatika katika Sana halafu zinachakaa haraka sana
 
Sasa TVS na BOXER injini zake ndo zipo imara au??? Hapo kuna mziki was timing chain........HIZO PIKIPIKI KUBWA NI NZURI SANA HASA KWA KAZI NA PILIKAPILIKA.....TENA UKIPATA KINGLION NDO UTAFURAHIA SANA.......ila kama unataka za luxury ndo unaweza nunua TVS au BOXER za mhindi...........MCHINA KWENYE INJINI YUPO VIZURI SANA...........
Mkuu timing chain inafanyaje Sasa?
 
Back
Top Bottom