Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Tuliambiwa SGR Dar to Morogoro ingeanza Dec mwaka jana, Stiegler's Gorge nayo kimya. Sio Msemaji wa serikali wala Polepole wala praise team wanaogusia, nini kimewapata.

Bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Tanga lilizinduliwa kwa mbwembwe tukaonywa atakayekwamisha atakiona, nani sasa amekwamisha. Je ule wimbo wetu wa kuhamia Dodoma umeishia wapi?

Tanzania ya viwanda imefikia wapi, juzi tuliambiwa tuna viwanda vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana, sijui hivyo vidogo sana ni vya wachoma mahindi?

Ndege zetu zimepaki? yaani.

Mambo ni mengi sana muda hautoshi.
 
....
Tanzania ya viwanda imefikia wapi, juzi tuliambiwa tuna viwanda vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana, sijui hivyo vidogo sana ni vya wachoma mahindi?

Hahahaa hivyo vidogo vidogo sana wanamaanisha vile vya kudanga. Maana shift ni kwa kila mshindo mtu anachukua wages yake.🤣🤣
 
Tulishaambiwa kuwa ukiwa na vyerahani 4 ni kiwanda hicho na wewe ni mwekezaji

In God we Trust
images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom