Ukinunua gari Zanzibar unatakiwa ulipe kodi ambayo ni differential.Mfano hiyo gari zanzibar ililipiwa kodi ya TZS 10,000,000/= iliponunuliwa kutoka Japan.Sasa mfano gari kama hiyo kuiingiza hapa Tanzania bara kutoka Japan kodi yake ni TZS 21,000,000/= basi wewe utalipa TZS 11,000,000/=(21,000,000-10,000,000) kwa sababu TZS 10,000,000/= tayari imelipwa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania.
Kwa hiyo wewe ulizia kwanza huko Zanzibar imelipa kodi ya kiasi gani iliponunuliwa kutoka Japan halafu ulizia gari kama hiyo ikiingia Tanzania bara kutoka huko japani huwa inatakiwa kulipiwa kodi kiasi gani kisha tafuta differential.