Saidi Abdallah Mikidadi mwenye miaka 33, mkazi wa
Dar es Salaam ambaye anakabiliwa na uvimbe mkubwa sana shingoni, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akisubiriwa kufanyiwa upasuaji mdogo kabla ya kusafiri nchini India kwa upasuaji mkubwa.
Akiongea jijini Dar, mdogo wa Saidi, Jundani Abdallah Mikidadi amesema Saidi alilazwa Muhimbili Jumatatu ya Aprili 13, 2026 kwa ajili ya maandalizi ya kufanyiwa upasuaji Jumatatu ya Aprili 20, 2026 na baadaye kupelekwa nchini India kwa ajili ya upasuaji mkubwa.
Jundani alisema kuwa, madaktari wa Muhimbili waliona ni vyema kama mgonjwa huyo akafanyiwa upasuaji wa awali Muhimbili na siku chache mbele apelekwe nchini India kwa lengo la kukamilisha matibabu yake.
Wakati huohuo, Saidi akizungumza kwa tabu akiwa kitandani kwenye Jengo la Sewa Haji Wodi 23, alisema anamwomba Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, mheshimiwa Dorothy Gwajima kumsaidia ili aweze kufanikisha safari yake ya nchini India kwa matibabu ya upasuaji mkubwa.
"Namwomba Waziri Dorothy Gwajima anisaidie.
Akiweza kama yupo Dar aje kuniona hapa Muhimbili nilikolazwa ili aamini kwamba nahitaji msaada wa pesa," alisema Saidi.
Akaongeza: "Nimekuomba wewe Waziri Gwajima uje kuniona au inisaidie kwa sababu nakukubali kwa jinsi anavyowajibika kuisiadia jamii bila kubagua wala kujali muda wako wa kujumuika na familia. Nitafarijika sana nikikuona laivu au ukinisaidia chochote mama yangu Gwajima."
Aidha, Saidi alisema kwa sababu bado anahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa Watanzania waliyoguswa na ugonjwa wake, kwa hiyo wanaweza kumtembelea Muhimbili kwenye Wodi Namba 23 Jengo la Sewa Haji ambako amelazwa akisubiri upasuaji wa Jumatatu ijayo.
Saidi alianzwa na uvimbe huo, Julai mwaka jana (2025). Alishaenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kitabibu Ilala (Amana). Akaenda Hospitali ya Rabininsia-Tegeta. Akaenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Lakini hakupata huduma kwa kile ambacho madaktari walisema haiwezekani kupasuliwa kwa hospitali za hapa Tanzania.
Januari 2026, akabahatika kuonwa na daktari mmoja wa Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, Prased Namani aliyefika kikazi Muhimbili ambaye alimwambia India wanaweza kumpasua na kutoa uvimbe huu ambao umekuwa ukitutumka (kuongezeka) kila siku.
Dokta Namani alimwambia ili afanikishe zoezi hilo zinatakiwa Tsh. Milioni 40 kama gharama za matibabu na usafiri kutoka Dar hadi India.
Ndipo hivi karibuni, madaftari wa Muhimbili walimchunguza kwa mara ya mwisho kabla ya safari ya India, wakasema ili asafiri salama salimini, itabidi afanyiwe upasuaji mdogo kwanza kabla ya kuanza safari ya kwenda India kwa upasuaji mkubwa.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Jundani Abdallah Mikidadi, upasuaji huo utafanyika ili kumuwezesha Saidi kumudu kusafiri kwenda nchini India kwa ajili ya upasuaji mkubwa ambao utafanyika kwenye Hospitali ya Apolo iliyopo katika Jiji la Hyderabad.
Alisema madaktari walishauri hivyo kwa sababu itakuwa vigumu mgonjwa huyo kumudu safari akiwa na uvimbe huo kamili na mkubwa.
Jundani alisema kuwa, hali ya Saidi kwa sasa ni mbaya sana kwa sababu uvimbe umeanza kuonesha 'mdomo' akimaanisha kuwa, unaweza kupasuka wakati wowote na ndiyo maana madaktari wa Muhimbili waliamua wamfanyie upasuaji mdogo kwanza.
Akaongeza kuwa, mgonjwa huyo anapumua kwa shida sana hali inayolazimisha kulala kwa muda wote.
"Baada ya upasuaji atapumzika kwa siku kadhaa tukiendelea kupokea michango. Ikikamilika tutafanya safari ya kwenda India," alisema Jundani.
Aliongeza kuwa, Saidi ameshalazwa Hospitali ya Muhimbili kwa ajili upasuaji wa Jumatatu.
Kuhusu maandalizi ya safari, Jundani alisema: "Kwa sasa tayari tuna viza ya kusafiria kikubwa ni gharama za safari na matibabu. Tunapokea mchango wa kiasi chochote. Hata iwe elfu moja, elfu mbili, elfu tatu. Zote hizo ni pesa na ni kubwa sana kwetu."
Jundani aliendelea kuwaomba Watanzania kuendelea kumchangia kaka yake ili aweze kufanikisha safari hiyo huku akimaliza kwa kusema; "MUNGU ABAWABARIKI WOTE."
Kwa Mtanzania uliyeguswa na ugonjwa wa Saidi na upo tayari kuchangia chochote, tuma mchango wako kwa simu namba; 0710 434416
NMB: 20310131829
(Jina: Jundani Mikidadi Abdallah).