Inategemea unataka uanzie level ipi ya hiyo biashara ila kama unataka uown ofisi iliyo complete itabidi uwe na large format printing machine ambayo hii ile ndogo kabisa inauzwa around million saba na nusu then uwe na kijana wa graphics ambae huyu ndio atakua anakusaidia kwenye kudesign hizo stickers pamoja na kufanya branding kwenye hizo pikipiki, bajaji na magari baada ya kupritiwa kwenye mashine.
Ila pia kama huna hiyo budget basi unaweza ukafungua ofisi tu na ukamuweka huyo mtu wa graphics yeye akawa anadesign then baada ya kudesign mnapeleka kazi kwa watu ambao wako na mashine wanaprint then ninyi mnafanya branding yaani kubandika kwenye chombo husika.
Bei za sticker huwa zinaprintiwa kwa mita na huwa zinatofautiana kulingana na material unayohutaji kwamfano contra vision huwa ni kuanzia 12k hadi 18k kwa square metre moja na pvc yaani hizi sticker za kawaida huwa ni kuanzia 7k hadi 9k kwa square metre na kadhalika na kadhalika.
Hapo ndio unaweza kuanzia then baadae utaadvance kwa kununua plotter, digital na kadhalika.