Thanks Kaka kwa hiki kipande! Inaonesha una maarifa na hii sekta. Naomba tumegee na part B. Na Kama hutojali na aina ya mikataba wanayoingia na Hawa underground
Mikataba ya muziki ipo mingi na inatofautuina lakini ni biashara kama biashara zingine nawewe unataka faida...
Traditionally walikuwa wanafanya ivi..
Unampata msanii mnasign mkataba,unampa advance tuseme mil5
Hiyo ni kwaajili ya vitu kama nguo na mambo mengine
Halafu unamgharamia kuproduce mziki i.e maproducer,video shoot etc.
Unagharamia promotion na marketing ya huo mziki
.
.
Ukishafanya hivo tuseme totally itakuwa mil 10 (mfano)
.
.
Baada ya hapo ataanza kuingiza pesa kupitia stream eg. Youtube,spotify etc.
Tuseme akaingiziza mil30
.
Hapo kwenye mkataba wewe utachukua gharama yako ile mil10 halafu inayobaki mnagawana na msanii
Kwahyo mil20 managawana
Sasa kuhusu asilimia ni makubaliano inaweza kuwa 50/50 au vyovyote lakini ni makubaliano....
Saivi kuna hizi 360 deals ambazo huishii kuchukua pesa kwenye mziki tu lakini kwenye kila kitu anachofanya kama shows,merchandise,matangazo etc. yan chochote anachofaidika kupitia mziki wake
in that sense pia lengo ni kurudisha gharama yako na kugawana faida...
.
.
.
Kuhusu part B hiyo ni upande wa marketing plan na promotion na distribution ya mziki hiyo haina formula,kila mtu ana formula yake lakini unaweza ukatafuta nyuki waliosoma marketing mkatengeneza asali
Au ukatumia uGenius wako ila partB sio lazma niseme kila kitu