Mwenye uzoefu na Toyota Raum new model

DIKASHWA

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
378
Reaction score
964
Naomba kujuzwa kuhusu TOYOTA Raum second generation (2004/6) ,nimeingia kwenye mitandao ya kuuza magari Japan kwa USD 1500-1600 ni CIF,nikaingia kwenye kikotozi chetu M5.3na ushee total ikaja kama nane na nusu unaweza kuingia barabarani
Kwa wataalamu wa magari
1) COMMON PROBLEM YA HILI GARI NI IPI
2) Avaibity ya spear zake na bei zake zipoje?
4) kwenye rough road inabehave vipi?
N.B mkuru baada ya kusema hamna nyongeza ya masurufu, nilikuwa naamka saa 10 kuwahi mwendo kasi sasa hamna haja tena ,najilipua japan nichukue mkoko mshahara wote niumalizie kwenye wese,maana hamna namna,
 
Hiyo gari navyosikia ni kuwa ipo very complex kwenye wiring yake ya umeme so ikicolapse ni kazi sana kuifix
 
Mimi nimeitumia hii gari kwa kipindi fulani, binafsi nachojua gari ni matunzo tu, ni kagari kazuri kwa kweli ukilinganisha na bei yake

Kuhusu mafuta wala usiwaze, ukiweka ya elfu 30 unazunguka jiji zima..

Spea kwa toyata hakuna shida kabsa, kariakoo kila kitu kipo tena kwa bei nzuri tu
 
Kama gari sio la luxury basi spea zake zinakuwaga cheap.hilo gari sio luxury spea zake ni simple tu. Tena Toyota spea zimetamalaki
 
Hii gari kuna siku ilinichezesha akili

Nilisimama mahala nikaweka Parking gear nikaizima kisha nikashuka

Basi nilipoingia tena ndani ya gari ile kuwasha chuma hakiwaki sehemu ya ignition nimeikuta ipo chini (kulia) yaan start kurudisha kushoto yaan Off ufunguo haurudi

Usukani haupindi, brake ina respond na gear shift ina respond ( dah ilinifikirisha kama dakika 5 ivi nikasema let me press shift lock kitu kika kubali aiseee mpaka leo sielewi ni nini kilifanya vile na tatizo lilikuwa nini

Labda mtalaam Extrovert brother unaweza guess issue ilikuwa nini ?
 
Itakuwa uliizimia kwenye gear labda mzee maana gari ikizimwa kwenye gear haiwakii kwenye gear mpaka uipeleke kwenye parking. Gari zenye shift lock huwa gear lever inajiloki haitembei kwenye reli bila kuiondoa kwenye lock na steering inajiloki na ufunguo hauendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…