Mwenyeji wa Dar Nakuhitaji Unisaidie: Natengeneza App Itakayosaidia Watu/Wageni Wa Dar Wasipotee

Mwenyeji wa Dar Nakuhitaji Unisaidie: Natengeneza App Itakayosaidia Watu/Wageni Wa Dar Wasipotee

Habari wana Ndugu,

Nilishawahi Kupotea Dar Nina Pesa Mkononi,Naona Daladala Zinapita Lakini Sijui Nipande Ipi Ili Nifike Ninapokusudia
Ghafla Paap! Naona Mdada Kasimama

Mimi:Mambo Samahani Dada (Huku Nikiwa na Kiaibu cha Kuuliza Ofkoz Kuna Kiaibu fulani Ukiwa Unauliza ) Hivi Hapa Nikitaka kwenda Kigogo Napanda Daladala Ipi?

Mdada:Mmmh Mimi mwenyewe Mgeni hapa Hata Sielewi
Mimi😱oh Poa Asante
(Nilitamani Kusikiliza Konda akipiga Debe Kigogo,rwanga lakin Mahali Nilipokuwa Nimesimama Hakukuwa Kituo rasmi Kwa Hio Daladala Zilikuwa zikipita Bila Kusimama Zinaenda Kusimama Mbele
Nikiwa nimezubaa Zubaa Ghafla Naona washikaji wawili warefu wamevaa nadhifu wanakuja kwa madoido Nikajisemea Hawa Lazima watakuwa waenyeji Ngoja niwavagae

Mimi:Inakuwaje Kaka
Mmojawapo😛oa
Mimi:Naulizia Daladala za Kwenda Kigogo
Mmojawapo😀aah Hapa Daladala za Kigogo kwa Hapaaa Hapa Hamna lakini sijui Sina Uhakika sana

Baada ya Kuulizia mtu wa Tatu Ndo Nikapata Maelekezo Mazuri lakini Tayari Nimeshafedheheka.
Kama Unaenda Mwisho wa Kituo Mara Nyingi Ni rahisi Kupata Daladala sababu Utangalia jina Mfano Makumbusho utaangalia Yenye Jina Makumbusho upande labda kama Hazipiti Ulipo lakin Vipi kama Unaenda Sinza,Magomeni,Ilala Hakuna daladala zilioandikwa Hayo Majina Pia Wewe Ni Mgeni Upo Nyumbani Haina Haja Ya Kwenda balabalani au kwa Majirani Kuuliza App Itakusaidia

Sasa Nilipata wazo Wazo La Kutengeneza App itakayosaidia Watu Kujua Wapande Daladala gani wakiwa Wanaenda Mahali Husika Au Wakiwa Wamepotea App Itawaelekeza Kutoka Hiyo Location Alioyopo (kwa Kutumia GPS) Apande Daladala Ipi Ili Afike Mahali Anapopakusudia Bila Kuuliza Uliza.

kama Ni Mgeni hata kama Mwenyeji wa Dar Es salaam anataka Kwenda Sehemu Fulani Haina Haja Ya Kuuliza Hapa Napanda Daladala Ipi Nifike Mahali Fulani ataingia Kwenye App Na App Itamuelekeza.

Nini nataka Kutoka Kwako Mwenyeji wa Dar Naomba Unisaidie Data.Jina La Daladala Na Route/Vituo Inavopita Mfano

Daladala: Makumbusho-Posta
Vituo inavopita:Mnazi Mmoja,Fire,Jangwani,Magomeni,Manzese,Urafiki,Shekilango,Sinza,Bamaga,Makumbusho

Daladala: M/complex- Mj/Coca
Machinga complex,Karume,Ilala,Kigogo,Rwanga,Mabibo,Urafiki,Shekilango,Sinza,Mwenge

Naomba Kwa Anayejua Daladala Zaidi anisaidie Kulingana Na Route Anayojua
Kinachotajikiwa Ni Jina la Daladala Imeandikwaje Kwa Mbele (Mf Makumbusho-Posta) na Jina La Vituo Inavopita Unaweza Usivipange kinaanza Kipi We Vitaje tu Vituo Muhimu.
Naimani Nitakusanya Data Nyingi Hapa JamiiForum


Nimeshaanza Kutengeneza Hii Ni demo tu Nitaongeza GPS na Mengineyo
Screenshoot.
Mtumiaji atasearch kutoka wapi kwenda Wapi.
Kumbuka Hiyo Ni demo Tu Nitaongeza Vitu

Very beautiful idea, why don’t you come to Dar and spend one week kwa mfano?
 
Hii nzuri sana. Wekana na Kiswahili.

Unapotaka kutengeneza app pata data kwenye source reliable.Nenda ofisi za Latra.Maana hao ndiyo wanaotoa route na kuzibadilisha. pia app yako inaweza kua inaupdate kila route inavyobadilika.

otherwise nenda kwenye stendi kubwa kubwa za dalala ukaone mwenyewe.mfano Gongo lamboto,mnazi mmoja,karikoo,mbagala,makumbusho,mhimbili,mbezi magufuli etc
Na mimi Nilikuwa Nafikiria Hivo Ila Nimekuja Jamiiforums Kwanza Ili Nipunguze Baadhi ya Route
 
Actually nafikiri mtu ambaye anaweza kutumia app yako means anaweza kutumia google maps na Uber so hawa ni washindani wako wa haraka haraka.

Kama waweza exploit weaknesses zao then utakua a step in the right direction.
Hujaelewa msingi Wa App.Msingi wa App Sio Kukupa Location Msingi wa App Ni Kukueleza Upande daladala Ipi.Mfano Nipo Manzese Nataka Kwenda Masaki App Itanielekeza Nipande Daladala za Mabibo-Makumbusho Nishuke Kinondoni Kisha Nipande Daladala za Masaki-Mawasiliano hyo Ndo Kazi Ya App
 
Very beautiful idea, why don’t you come to Dar and spend one week kwa mfano?
Mimi Ni Mkazi Wa Dar.Kuwa Mkazi Haimaanishi Unajua Kila Route Ndo Maana Nikaja Huku JamiiForums Kusaidiwa Naamini Kuna Wenyeji pia
 
Safi sana kijana Bora Yako Inaashiria ELIMU uliyopata Ina msaada kwako Mkono wa bwana uwe pamoja na ww
 
Mm ndo natumiaga

Mi pia sijawahi kufeli napokwenda nikitumia google maps nafika. Kasoro njia za mitaa tu ndani ndani ndo natumia boda boda ila road to road google maps imecover fresh hadi majina ya vituo yapo.
 
Wazo zuri sana na litasaidia wengi, kwani wanaotoa hizo route huwezi kuwafikia hao LATRA?
Nafikiri wao wangekupa kila msaada unaotaka
Ila sina uhakika nimewaza tu
 
So hi App the End user ni abiria wa daladala.?
 
Back
Top Bottom