PreGE2025 Mwenyekiti ADC: CCM acheni kuwafanya Wasanii na Wanafunzi Vyuo Vikuu kuwa wasemaji wa chama

PreGE2025 Mwenyekiti ADC: CCM acheni kuwafanya Wasanii na Wanafunzi Vyuo Vikuu kuwa wasemaji wa chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Taratibu mwanga unaanza kuonekana! Chawa wanatagiwa kupigwa vita pande zote, yaani vijana baada ya kuwa mstari wa mbele kuokoa taifa ndio tunakuwa wa kwanza kuzamisha meli!

#PigaVitaUchawa #KataaUchawa

===

Mwenyekiti wa chama cha ADC Shabani Itutu amesema;

Wasanii na wanafuzi wa vyuo vikuu wamegeuka kuwa chawa, asema serikali iwaache wanafunzi wasiwe kuwa wasemaji wa chama ili tupate wanafunzi watakaokuja kusaidia taifa.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Vile vile kwa wasanii ambao karibu wote wamegeuka kuwa machawa wanakuwa hawana msaada kwa taifa, wakiwa wamesahau kazi yao muhimu ya kuelemisha na kufungua macho wananchi, akiongeza tunakosa wasanii konki kama Remmy Ongala ambaye nyimbo zake zilikuwa na tija kwa maslahi ya nchi.

Shabani ameitaka serikali kutowafanya wanunzi na wasanii kutokuwa wasemaji wa chama, ambako wakati huu wanafunzi vyuo vyote wanatamani kuwa machawa.

​
 
Ni lazima wawe chawa kwa sababu hiyo ni fursa, ukiwa chawa mzuri ajira nje nje na mkwanja wa kutosha.
 
Kuanzia sasa usipokee simu usizozijua, maana umenena kwa lugha japo mburula hawatakuelewa.
 
Akifanya mahojiano katika kipindi cha Medani za Siasa Star TV Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic change (ADC) ametoa wito kwa Serikali kuacha kuwatumia wanafunzi na wasaanii kwenye masuala ya siasa.

"Wasanii na wanafunzi wa vyuo vikuu acheni uchawa nyie sio wasemaji wa CCM, na CCM tuwaombe sana acheni wanafunzi wasome na wasanii wafanye kazi zao msiwafanye kuwa wasemaji wenu" SHABANI ITUTU - M/KITI - ADC.
 
View attachment 3287846

"Wasanii na wanafunzi wa vyuo vikuu acheni uchawa nyie sio wasemaji wa CCM, na CCM tuwaombe sana acheni wanafunzi wasome na wasanii wafanye kazi zao msiwafanye kuwa wasemaji wenu" SHABANI ITUTU - M/KITI - ADC.
Vyuu vikuu tunategemea kuwe na wasomi ambao wanajua kuchambua mambo na wenye misimamo thabiti na waona mbali. Sidhani kama kuna haja hata ya kuaambia kwa sababu wao ndiyo walitakiwa kujua kuliko mtu mwingine yeyote. Wakikubali kutumika vibaya basi hasara ni yao.
 
Back
Top Bottom