Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Mwenyekiti BAZECHA - James Haule alipoulizwa kuhusu busara itumike kuponya majeraha CHADEMA, Haule wamesema;
BAZECHA ndio wenye wajibu wa kuponya majeraha chamani, nataka niwathibitishie tulishakaa na Mbowe, Lissu pamoja na Mnyika, kwakuwa watu walidhani wamekanyagana tulitoa nafasi ya watu waje kujieleza juu ya kukanyagana kwao, lakini hakuna aliyejitokeza matokeo yake tumesikia tu mtu ameshuka kwenye basi, haijulikani anakwenda wapi. Kwahiyo tunasubiria na sisi tunaendelea kufanya kazi na nnataka niwahakikishe baada ya BAZECHA kuchunguza - chama kipo imara kuliko wakati mwingine wowote, habari inatema uchafu acha bahari iwe safi.
Hivyo nitoe wito kwamba anayeshuka kwenye gari amefika safari yake sababu safari ni siasa na ina mwendo mrefu na watu watachoka njiani, na kuna watu wengine watafika mahala wataamua kushuka na kubaki hapo hapo waliposhukia. Pengine hata nchi ya ahadi wanayotaka kwenda, wasifike. Kwahiyo tunawapa mkono wa safari njema huko waendako, CHADEMA tuko salama tunaendelea kupiga mwendo.