McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kanda ya Kati na mwanachama mwanzilishi wa chama hicho, Acquilin Magalambula, amesema amesikitishwa na ziara zinazoendelea kufanywa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, katika Kanda ya Serengeti.
Magalambula ameeleza kutoridhishwa na kauli alizodai Heche alizitoa alipokuwa Mugumu na Nyamongo, akimtaja Mwenyekiti wa chama aliye gerezani kama makamu mwenyekiti, akisisitiza kuwa kiongozi huyo alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kikatiba Januari 2015.
Amesema Mwenyekiti huyo bado ndiye kiongozi aliyechaguliwa kwa mujibu wa taratibu za chama, huku Heche akiwa makamu mwenyekiti anayetekeleza majukumu yake wakati mwenyekiti hayupo.
Aidha, Magalambula amemshauri Heche kusoma kitabu The 48 Laws of Power, akisisitiza umuhimu wa kutambua mipaka ya uongozi na kuepuka kauli zinazoweza kutafsiriwa kama kujitwalia nafasi ya mwenyekiti wa chama.
Akizungumza na waandishi wa habari, Magalambula ametoa onyo kwa Heche akimtaka kutambua nafasi yake ndani ya chama na kuheshimu uongozi uliopo, akisisitiza kuwa yeye ni makamu mwenyekiti na si mwenyekiti wa CHADEMA.