BAZECHA Pwani wanaongea na Waandishi wa Habari
Mwenyekiti BAZECHA - James Haule
Ni kwa mara ya kwanza Kanda ya Pwani kuongea na waandishi wa Habari, tumekuwa tukifatilia kwa ukaribu mazingira halisi yaliyopelekea cnhi yetu kufikia siasa za kikatili ambazo zinaendeshwa na serikali ya CCM.
Wazee wa BAZECHA wanaalni vikali sana hatua zote zilizojitokeza katika kuharibu mahusiano ya watanzania, upendo na haki pamoja na uhuru wa watanzania. Hatukutarajia kisiwa cha amani kuwa sehemu ya ukatili, kutozingatia utu, viongozi wa serikali wanaona ni jambo la kawaida kufanya ukatili kwa raia wema. Wahanga wakubwa ni viongozi, na wananchama wa CHADEMA.
Kutokana na yanayoelendelea BAZECHA tumeamua tutoke hadharani na kukemea vikali dhidi ya ukatili, ukandamizaji, dhulma ya haki na damu za wanachadema ili vitendo hivi visiendelee katika nchi yetu.
CHADEMA kupitia BAZECHA tunatoa wito kwa Rais Samia kutoka hadharani kwakuwa yeye ndio mfariji wa taifa kulieleza taifa kwanini watanzania wananyanyasika katika ardhi yao na amechukua hatua gani ili kulinda haki uhuru na demokrasia katika taifa la Tanzania.