Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga (MCC) akabidhi Milioni 2 kwa wauza samaki ili kukuza mtaji

Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Tanga (MCC) akabidhi Milioni 2 kwa wauza samaki ili kukuza mtaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Tunaendelea kwenye episode nyingine ya rushwa ambayo huwezi kuona TAKUKURU wakiipigia kelele.

====

Screenshot 2024-11-20 200538.png

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimeiagiza Serikali ya Wilaya ya Pangani kuhakikisha kinatenga eneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kuuza Samaki wa kukaanga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Mwenyekiti wa Chama hicho tawala Mkoani Tanga (MCC) Ustaadh Rajabu Abdarahman Abdallah ametoa maagizo hayo katika ziara yake wilayani humo alipopata fursa ya kutembelea Wafanyabiashara wadogo kuzungumza nao ili kujua changamoto zinazowakabili.

Soma Pia: Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga Achangia Milioni 10 Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mwembeni

Screenshot 2024-11-20 200546.png

Katika ziara yake hiyo, Ustaadh Rajabu Abdarahman Abdallah amesema, baada ya kuwatembelea amejikuta akisononeka kutokana na mazingira wanayotumia ku ndesha shughuli zao kutokuwa rafiki na hivyo kuonekana kana kwamba wametelekezwa.

"Nilipita hapa usiku nikaona nimesononeshwa na mazingira mnayofanyia biashara ni kama mmetupwa mkono. Hivyo niagize Serikali iwatafutie eneo japo Pangani kuna changamoto ila naamini litapatikana" alisema Ustaadh Rajabu Abdarahman Abdallah.

Pamoja na kutoa maagizo hayo, pia Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tanga ameeleza kwamba ipo haja kwa Wajasiriamali hao wadogo wadogo kutambuliwa na kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kusaidiwa kirahisi.

"Diwani hakikisha Wafanyabiashara wote kwenye Kata hii ya Pangani Mashariki wanatambuliwa, hata wale wa magharibi watambuliwe itakuwa rahisi kusaidiwa" amesema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga.

Kuhusu suala la changamoto ya mitaji kwa Wajasiriamali wanapouza Samaki wanakaanga Pangani Mashariki, Ustaadh Rajabu Abdarahman Abdallah aliwapatia fedha taslimu Shilingi Milioni 20 ili kusaidia wakinamama nane (8) kuimarisha biashara zao.
 
Kichwa cha habari umesema 2M ila ndani ya maelezo ni 20M so tushike lipi????
 
Takrima haina tofauti na rushwa. Na yalivyo mazuzu yatakubali kudanganyika.
 
Back
Top Bottom