Pre GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Kaskazini: Nitawashughulikia wote wasiomkubali Lissu

Pre GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Kaskazini: Nitawashughulikia wote wasiomkubali Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha kuleta hoja na kuishia kuipotosha.
Leta tafsiri tofauti na alichosema Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini kwenye hiyo clip?Au alikuwa anaongea kiiraqw?
 
Mwenyekiti CHADEMA Kanda Kaskazini Wakili Welwel wakati akifungua kikao kazi kilichohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Kamanda John Heche kilichofanyika Siku ya jana Equator Hotel Arusha amesema kuna wanachadema bado wanaugulia maumivu kama vile wamefiwa. Anahoji ni maumivu gani ya mwezi mzima yasiyopona baada ya uchaguzi.

Ametishia kuwashughulikia ikiwemo kuwapa kesi ya uhaini kwenye chama.

View attachment 3246768
Wote ambao mna maumivu ya chama Cha harakati karibuni chama dume CCM huku ni furaha ,amani,utulivu na kuendeleza kushika dola
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mawazo tofauti yasiyovumilika ni yapi?

Uchaguzi ulifanyika kwa uhuru mkubwa. Viongozi ambao wengi waliwataka, walikwishapatikana. Kuwakataa viongozi waliopatikana kidemokrasia na kwa kufuata kanuni na taratibu zote za chama, ni kukihujumu chama. Anayehujumu chama ni adui wa chama.
nini maana ya uchaguzi
 
Nchi hii ni muhimu Serikali ikafuta vyama vingine vibaki vyama vitatu vikubwa pekee, iwekeze nguvu ya kutosha na vipewe pesa kusaidia Nchi kukuza DEMOKRASIA na maendeleo
Naunga mkono hoja.
 
Mwenyekiti CHADEMA Kanda Kaskazini Wakili Welwel wakati akifungua kikao kazi kilichohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Kamanda John Heche kilichofanyika Siku ya jana Equator Hotel Arusha amesema kuna wanachadema bado wanaugulia maumivu kama vile wamefiwa. Anahoji ni maumivu gani ya mwezi mzima yasiyopona baada ya uchaguzi.

Ametishia kuwashughulikia ikiwemo kuwapa kesi ya uhaini kwenye chama.

View attachment 3246768
Huyu bwege anadhani kwa kuropoka hivi anakisaidia chama na kwa upeo wake sijui atawasghuliaje wasiompenda Mzee wa Ubelgiji?
Kwa trend hii CDM haitapata hata Diwani mmoja seuze mbunge Chugga.
 
Ningependa kujua Heche alisema nini. Hauwezi kulazimisha maridhiano. Badala ya vitisho vya kipuuzi kama hivi uongozi unatakiwa kufanya juhudi za ziada kuwadhihirishia wale ambao hawana imani nao kuwa wamekosea. Badala ya vitisho wawakumbatie, wawape nafasi na wasikilize hoja zao.

Hamna chama kilicho hai ambacho hakitakuwa na tofauti ya mitizamo. Kulazimisha kukubalika ni u dikteta. Inaleta swali kuwa watu kama hawa wakiwa na dola, watawashughulikia vipi wale wanaotofautiana nao. Ni kauli za kukanwa mapema sema kwa kusisitiza kuwa CDM ni tent kubwa na sio dhambi mtu kuuguza maumivu au kutofautiana na uongozi.

Amandla...
 
Huyu kiongozi alishinda kwa 51% ambayo inamaanisha kuwa 49% hawakumkubali. Inabidi atambue hilo na afanye kazi ya kuwabadilisha mawazo hao 49%. Hivyo hivyo kwa Lissu.

Amandla...
 
Shida ni kuwa ,ukihama CHADEMA unaenda wapi!

Nchi hii ni muhimu Serikali ikafuta vyama vingine vibaki vyama vitatu vikubwa pekee, iwekeze nguvu ya kutosha na vipewe pesa kusaidia Nchi kukuza DEMOKRASIA na maendeleo
Suluhisho ni serikali kuruhusu mgombea binafsi, vyama vitajifia vyenyewe na huu udikteta wa vyama utazikwa.
 
Shida ni kuwa ,ukihama CHADEMA unaenda wapi!

Nchi hii ni muhimu Serikali ikafuta vyama vingine vibaki vyama vitatu vikubwa pekee, iwekeze nguvu ya kutosha na vipewe pesa kusaidia Nchi kukuza DEMOKRASIA na maendeleo
Kuvunja vyama vilivyoanzishwa kwa lengo la yawadanganya WB & IMF inakuwa si rahisi...ndio maana ndani ya vyama kumejaa mizaha.Demokrasia ya kweli inaleta maendeleo,maana ni Hoja tu ndizo zinazoshindanishwa.2049 wengi wao
Watakuwa wazee sana na hivyo hiyo mentality itakuwa haina nguvu.
 
Mwenyekiti CHADEMA Kanda Kaskazini Wakili Welwel wakati akifungua kikao kazi kilichohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Kamanda John Heche kilichofanyika Siku ya jana Equator Hotel Arusha amesema kuna wanachadema bado wanaugulia maumivu kama vile wamefiwa. Anahoji ni maumivu gani ya mwezi mzima yasiyopona baada ya uchaguzi.

Ametishia kuwashughulikia ikiwemo kuwapa kesi ya uhaini kwenye chama.

View attachment 3246768
Yaan mwenyekiti wa Taifa hakubaliki?

sasa kama ni hivyo,
Makamu mwenyekiti si ndio atakua anaonekana kama mzururaji tu 🤣
 
Shida ni kuwa ,ukihama CHADEMA unaenda wapi!

Nchi hii ni muhimu Serikali ikafuta vyama vingine vibaki vyama vitatu vikubwa pekee, iwekeze nguvu ya kutosha na vipewe pesa kusaidia Nchi kukuza DEMOKRASIA na maendeleo
eti ng'we ng'we ng'we,
ati vipewe pesa? Ya nini, mmezoea konyagi na nyama ee?🐒
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Samwel Welwel, amesisitiza kuwa chama hakitavumilia makundi yanayopinga uongozi uliopo madarakani.

Welwel amesisitiza mshikamano ndani ya chama na kuonya kuwa viongozi wa mikoa na majimbo ambao bado wanashikilia makundi ya upinzani dhidi ya uongozi uliopo kuwa xhawatafumbiwa macho.

“Hata mimi nilikuwa mstari wa mbele wakati Freeman Mbowez anakwenda kuchukua fomu. Sasa uchaguzi umekwisha, tunapaswa kumuunga mkono Tundu Lissu kama Mwenyekiti wa chama Taifa na John Heche kama Makamu Mwenyekiti wa Bara. Mtu yeyote anayekataa kuutambua uongozi huu hana nafasi ndani ya chama,” alisema Welwel.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, kutotambua uongozi ni sawa na uhaini, hivyo ni lazima wanachama waungane kwa ajili ya kuimarisha chama na kujiandaa kwa mapambano dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Welwel pia amekosoa wanachama wanaoendelea na malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa chama, akifananisha hali hiyo na maombolezo yanayodumu kwa muda mrefu kupita kiasi.

“Hivi kweli mwezi mzima umepita bado machungu yapo tu? Hata ukifiwa na mke au mume, siku tatu zinatosha kuvunja matanga. Sasa kwa nini matanga ya uchaguzi yanaendelea?” alihoji.

Mwisho, amewataka wanachama wote wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini kurudi pamoja na kujenga chama kwa mshikamano, akisisitiza kuwa huu si wakati wa migawanyiko bali wa kuimarisha chama kwa ajili ya mapambano ya kisiasa yajayo.

Kawaida sana

Ally Hapi hakuwa Team Sukuma gang lakini baada ya kuteuliwa alikuwa zaidi ya Sukuma gang
 
Mwenyekiti CHADEMA Kanda Kaskazini Wakili Welwel wakati akifungua kikao kazi kilichohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Kamanda John Heche kilichofanyika Siku ya jana Equator Hotel Arusha amesema kuna wanachadema bado wanaugulia maumivu kama vile wamefiwa. Anahoji ni maumivu gani ya mwezi mzima yasiyopona baada ya uchaguzi.

Ametishia kuwashughulikia ikiwemo kuwapa kesi ya uhaini kwenye chama.

View attachment 3246768
Thanks
 
Back
Top Bottom