Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Kilindi, Mathias Cosmas (maarufu kama Mpendakula), amejibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kwa kile alichodai kuwa ni kutolewa kwa lugha ya dhihaka ya kuitwa "mbwa."
Akizungumza mbele ya wanahabari, Mathias amesema "kuitwa Mbwa ni Sifa" na kuongeza kuwa haoni neno hilo kama tusi bali ni sifa, kwani kazi ya mbwa ni ulinzi, usalama na kunusa maovu, huku akioanisha kazi hizo za Mbwa na wajibu wake katika kulinda chama.
Amekosoa matumizi ya lugha kali na vitisho kutoka ngazi za juu za uongozi, akibainisha kuwa uongozi bora haujengwi kwa mabavu au vitisho bali unahitaji hekima na busara.
Aidha, amerejea kauli ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, aliyesisitiza matumizi ya busara ndani ya chama, akitolea mfano wa hekima ya uongozi wa Mfalme Suleiman.
Soma pia https://www.jamiiforums.com/threads...a-john-heche-asema-haogopi-kufukuzwa.2452452/