Mwanasiasa mkongwe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Imma Saro, ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho baada ya kukitumikia kwa zaidi ya miaka ishirini, akieleza kuwa amefikia hatua ya kubadilisha jukwaa la kisiasa kwa dhamira ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa njia tofauti
Kupitia taarifa yake kwa wanachama iliyotolewa Juni 30, 2025, Imma Saro amesema ameondoka kwa moyo wa shukrani na unyenyekevu mkubwa, akieleza kuwa hatua hiyo ni matokeo ya tafakari ya kina juu ya mwelekeo wake wa kisiasa na dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa njia nyingine
Saro alitumikia kama Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Wilaya kati ya mwaka 2010 hadi 2019, kabla ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Siha kuanzia 2018 hadi 2025. Ametaja utumishi wake ndani ya chama kuwa wa uaminifu na uzalendo, akisema amejifunza mengi na atabaki na heshima kubwa kwa wanachama na viongozi wote aliowahi kufanya nao kazi
Hata hivyo, amesema siasa siyo lengo bali ni jukwaa la kuwatumikia wananchi, na kwamba uamuzi wake wa kuondoka umechukuliwa kwa utulivu na uhuru wa dhamira, bila kuwepo na hasira wala hofu
“Uamuzi huu si wa hasira wala hofu, bali ni hitimisho la tafakari ya kina juu ya namna bora ya kuendelea kuwatumikia watu wa Siha na taifa kwa ujumla”, amesema Imma
Saro pia ameomba radhi kwa yeyote ambaye aliwahi kumkosea katika safari yake ya kisiasa, akisisitiza kuwa siasa siyo uadui bali mabadiliko ya fikra, huku utu, upendo na heshima vikibaki kuwa misingi isiyotikisika.
Amehitimisha kwa kumtanguliza Mungu na kuwatakia heri wanachama wote wa CHADEMA waliobaki, akisema ataendelea kuwatumikia watu wa Siha na Tanzania kwa ujumla katika mazingira mapya ya kisiasa atakayoyachagua