Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya, amesema mafunzo yanayotolewa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni suluhu muhimu katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana nchini, hususan kizazi cha Gen-Z.
Maganya ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya viongozi wa jumuiya hiyo katika Makao Makuu ya VETA jijini Dodoma, amesema kuwa kupitia mafunzo ya ufundi stadi, taifa linaelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Amesema wazazi wana wajibu mkubwa wa kuwaelekeza vijana kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi na kuwajengea misingi ya kujiajiri, ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea kiuchumi.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata ajira.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema VETA imeongeza vyuo zaidi ya 30 katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini, na kufikia jumla ya vyuo 80, huku vyuo 65 vikiendelea kujengwa kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ujuzi na ajira kwa vijana.
Kasore amesema udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 61,000 hadi 86,000 kwa mwaka kwa kozi za muda mfupi na mrefu, huku serikali ikigharamia kwa kiwango kikubwa ada za masomo kwa wanafunzi wa VETA.
Amefafanua kuwa serikali imetumia takribani shilingi bilioni 7.2 kununua vifaa vya kisasa vya kujifunzia kwa vyuo vya zamani ili viendane na mabadiliko ya teknolojia, ambapo zaidi ya vyuo 60 vimenufaika na vifaa hivyo.