Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa (CCM), Fadhil Maganya amesema kilichotokea Oktoba 29 wakati wa uchaguzi kwa baadhi ya vijana kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali ya nchi, hakikuwahi kutokea, hivyo Rais Samia kutoa msamaha kwa baadhi ya vijana waliofanya vurugu hizo kwa kufuata mkumbo sio uoga kama baadhi ya watu wanavyofikiri
Akizungumza Leo Novemba 15 jijini Dodoma, amesema alichofanya Rais ni kutibu maumivu kwa kutoa msamaha kwa baadhi ya vijana walioshiriki vurugu hizo pasipo kufahamu wanachokitenda.
"Mheshimiwa Rais angeweza kufanya chochote anachoweza. Machafuko haya yamewahi kutokea nchi mbalimbali na hawakuwahi kuchukua hatua kama alizochukua mheshimiwa rais kwa kutoa msamaha" amesema Maganya
Maganya amesema kuwa lengo kuu la hatua hiyo ni kuifanya Tanzania kusonga mbele kama taifa moja lenye umoja, mshikamano na heshima baada ya kipindi cha uchaguzi.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi, viongozi na jamii kwa ujumla kuendelea kuwaongoza vijana kutambua thamani ya amani na kuachana na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi