Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi CCM Ileje adaiwa kuuawa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chitete wilayani Ileje, mkoani Songwe, Harison Mwampashi (62) amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na watu wasiojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji, hicho Joseph Mwashitete amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano Machi 12, 2025 saa tatu usiku katika Kijiji cha Ntembo akiwa anatoka kilabuni.

Mwenyekiti huyo ameliambia mwananchi kuwa alipokea taarifa za kifo cha mzee huyo kutoka kwa Joseph ambaye ni mtoto wa marehemu, aliyemweleza kuwa aliuona mwili wa baba yake barabarani.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Songwe, Augustino Senga amesema bado hajapokea taarifa hizo kwa sababu yupo nje ya ofisi, atafuatilia tukio hilo ili atoe taarifa rasmi.
1741874138011.png
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chitete wilayani Ileje, mkoani Songwe, Harison Mwampashi (62) amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na watu wasiojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji, hicho Joseph Mwashitete amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano Machi 12, 2025 saa tatu usiku katika Kijiji cha Ntembo akiwa anatoka kilabuni.

Mwenyekiti huyo ameliambia mwananchi kuwa alipokea taarifa za kifo cha mzee huyo kutoka kwa Joseph ambaye ni mtoto wa marehemu, aliyemweleza kuwa aliuona mwili wa baba yake barabarani.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Songwe, Augustino Senga amesema bado hajapokea taarifa hizo kwa sababu yupo nje ya ofisi, atafuatilia tukio hilo ili atoe taarifa rasmi.View attachment 3269276
Safi sana
 
Back
Top Bottom