Mwenyekiti wa Bodi ya Kampeni ya Kitaifa ya Mama Asemewe Alawi Abdallah amewahakikishia Watanzania kuwa nchi yao ni tulivu na yenye usalama mkubwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025
Alawi amebainisha hayo Mkoani Kagera wakati akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kuwa ametembea kwenye Mikoa mbalimbali nchini na kukutana na Vijana kutoka kwenye makundi mbalimbali, wakieleza shauku yao kuhusu uchaguzi Mkuu na wakikiri kutotambua ama kuhamasika kuhusu nia ovu ya maandamano inayosambazwa na watu wachache kwenye Mitandao ya kijamii
"Mimi nawaambieni nchi yetu ipo salama na watu wana ari ya kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan suala ambalo linadhihirisha kuwa wanaopiga kelele mitandaoni wanapoteza muda wao na hawana kazi ya kufanya. Naomba niwaalike waje Mama asemewe tuzisake kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan." Amesema Bw. Alawi
Aidha Alawi ameeleza kuwa anawafahamu watanzania wote wanaoishi Ughaibuni wakifanya shughuli za kuhamasisha wananchi kufanya vurugu, wengi wao wakitokea Japan na Ubelgiji na kusema watu hao wamekuwa pia wakiwafadhili baadhi ya Vijana wa Kitanzania kufungua akaunti feki za Mitandao ya kijamii na kuanza kuuonesha umma kuwa wapo tayari kwaajili ya ushiriki wa maandamano wanayopanga kuyafanya Oktoba 29, 2025
Soma pia GE2025 - Vijana wa mama asemewe watinga Singida kuhamasisha vijana kushiriki uchaguzi mkuu