Mwenyekiti Kawaida ahimiza Uzalendo, Umoja na Mshikamano kwa Wasomi Mkoani Dodoma

Mwenyekiti Kawaida ahimiza Uzalendo, Umoja na Mshikamano kwa Wasomi Mkoani Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
🗒️ 08 June 2024
📍UVCCM HQ

Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali kawaida (MCC) amehimiza Uzalendo, Upendo, Umoja, na mshikamano, Miongoni mwa wasomi na kujitoa katika kutekeleza Majukumu yao na ya kukijenga Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya zake zote na Serikali Kwa ujumla.

Komredi Kawaida ameyasema hayo Alipokua anazungumza na Wasomi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dodoma tarehe 08 Juni, 2024 ambapo alikua Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Seneti hiyo.

Aidha, Komredi Kawaida amewapongeza Wasomi Wote Kwa Kufikia hatua muhimu ya kuhitimu Masomo yao Vyuoni kwa Mwaka 2024

Komredi Kawaida amewaeleza wasomi hao kuwa UVCCM chini ya Uongozi wake ina Mpango kabambe wa kuzisogeza fursa Mbalimbali karibu na Vijana kwa kutengeneza namna nzuri ya fursa hizo kuweza kufikika Kwa urahisi.

Pia Komredi Kawaida amesema Umoja wa Vijana wa CCM umejipanga kuhakikisha Vijana wote wanaojitoa Kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi wanatambulika na kunakuwa na mfumo rasmi wa kuwatambua pamoja na kuhifadhi taarifa zao zote zitakazoisaidia jumuiya pale watakapohitajika katika kuwapa fursa au kwa matumizi ya Chama Cha Mapinduzi.

Komredi Kawaida amewasihi Vijana Wote Wasomi wa Seneti mkoa wa Dodoma Kuendelea kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuyasema yale yote Mazuri yanayofanyika katika Serikali ya awamu ya sita.

Mwisho, amewahimiza Vijana wote Wenye uwezo Kujitokeza kwa wingi kugombea katika chaguzi za Serikali za mitaa 2024 na amewatoa hofu kwani Chama Cha Mapinduzi kipo na kinatoa fursa za Uongozi kwa Vijana hivyo atawapa ushirikiano wakutosha katika kila hatua ili kuhakikisha Vijana wanaweza kushika nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo za 2024/2025

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM- Taifa

WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.20.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.20(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.21.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.22.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.23.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.23(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.24.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-08 at 17.52.26(1).jpeg
 
Back
Top Bottom