Kuniita mpambe ni kunionea sana au kutokusoma maandiko yangu na kuyaelewa.
Ni kweli ni wakati wa Mbowe kupisha wengine kuongoza mapambano, lakini kugombea kwake hajavunja katiba na pia bado anastahili kupendwa na kuheshimiwa kwa aliyofanya kwa Chadema, upinzani na Tanzania kwa jumla.
Ila ni wazi kuwa hakuna wanafiki wakubwa duniani kufikia kiwango cha CCM, wao walikuwa wanapiga kelele oo Mbowe ni sultan hataki kutoka madarakani nk. Sasa Chama kinataka kumpumzisha aingie kamanda asiyeshindwa Lissu na eti wanamtaka Mbowe kwa mbinu zote.
Wakae kwa kutulia hayo ni ya Chadema