TANZIA Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE

RIP DR. Mengi mtu wa watu.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo tulikualika kwenye Graduation yetu ya kidato cha nne, ukakosa nafasi ila ukatuma mwakilishi - nakumbuka Lori kadhaa za Soda toka Bonite zikiingia shuleni.

Aisee Tulioga soda.... huku tukiimba IPP cares for you...!!!
 
Pumzika kwa amani Dr Mengi. Nimeusoma wasifu wa Dr Mengi nikakumbuka Kitabu kimoja aliandika Albert Nyaluke Sanga Chapter ya kwanza inaelezea kuhusu kurefusha wasifu wako.
Dr Mengi ana wasifu ambao unausoma mpaka unasisimka na kujiona unacheza makida makida hapa duniani. Ni mtu amekufa kwa sauti kubwa, ni mtu amekufa na dunia inajua amekufa, mpaka ubalozi wa Marekani walitoa salam za rambirambi.
Hakikisha unapokufa kama sio dunia ijue basi hata Tanzania ijue. Usife kimya kimya😢
 
Raha ya milele unipe Ee BWANA, na mwanga wa milele uniangazie, nipumzike kwa amani.
 
Nakumbuka ni majuzi tu alitoa ahadi kwa Serengeti boys, japo walimuangusha !!. Makanisa na misikiti nayo imepoteza kwa kuondokewa na Dr Reginald Mengi. Tusisahau jamii ya walemavu. Inayobaki ni Ile mijitu yenye roho mbaya na chafu isiyojali utu na maisha ya wengine.

R I P Dr R. Mengi
 
R.I.P Mzee Mengi. Watu wenye uhitaji maalum watakosa mengi.
 
Pamoja na madhaifu tunayokuwa nayo binaadam, na bila kujali mambo mengi yanayoambatana na aina ya kazi alizoshiriki kujiendeshea maisha; Bwana Mengi kwa maoni yangu alikuwa ni Mzalendo, mTanzania wa kweli kweli. Aliipenda Tanzania kwa juhudi zake alizozifanya.

Heshima kwako Dr Mengi kwa kazi kubwa uliyoifanya hapa duniani.

Mungu amlaze mahali pema katika mapumziko yake.
 
PIA SISI BINADAMU TUWE NA BUSARA KUNA WATU WANACOMMENT HUMU MPAKA UNASHANGAA WAKATI YEYE AKIFA SIJUI KAMA HATA KUNA JEMA MOJA WALIOBAKI WATALISEMA JUU YAKE KWANI AMEJAA UCHAFU MTUPU.
 
Watu wema wanaondoka,tumebaki "sisi" mashetani!May the soul of our beloved Reginald Abraham Mengi rest in peace!
Inatia huruma inahuzunisha inasikitisha nimewazaa nikajiuliza kipi kinaendelea nyuma ya pazia itakuwa kweli vifo LAKINI tunachochote tunachotakiwa kujifunza maana matajiri niwachache tuliwategemea kwa ajira, kodi, misaada, serikali inalakujifunza sio mambo yaende tu then watu waendelee na porojo na mikomesho jamii ndio itaathirika.

unakuta na matajiri waliobaki nao wamefilisika mara nao wana shida zao tutajiweka rehani kwa nchi gani
Kama kuna chuki au mambo mabaya tusifanye kwa watu wenye michango ya jamii nikuwaongezea stress kulibeba taifa la tanzania si kazi rahisi shida ni nyingi mno, tuheshimu akili za wengi waliofanikiwa na si kuwapa maudhi.

Lakini pia jamii ijifunze kuwajibika na Matajiri wengine kuiga mfano wa mchango waliotoa wenzao waliotangulia mbele za haki la sivyo inchi itapoteza mwelekeo ndani ya sekunde baada ya matukio flani flani.
 
Kwanza poleni Familia, Ndugu na marafiki wa mpendwa wetu R.A. Mengi. Kweli Mengi alipendwa na Watanzania. Taarifa zilivyopatikana asubuhi ya leo wengi hawakuamini masikio yao kuwa Mengi hatunaye. Wazee, Akina Mama, vijana wameguswa sana na taarifa hii wakikumbuka misaada aliyokuwa anatoa bila kujali kabila rangi,eneo analotoka mtu. Mengi alipendwa sana Watanzania wote na upumzike kwa amani.
 
We jamaa una roho mbaya sana! Mbona yule mama alizikwa kwa heshima zote kuanzia Dar, moshi kkkt hadi machame? Ulikuwa unafatilia mazishi yake kweli?
Siyo roho mbaya nimesema hivyo na itabaki hivyo. Narudia hakuna heshima kama ya Mzazi mwenza. She was not even mentioned. Acha kabisa. As a long time married man with my beloved wife ambaye anafanya kazi kubwa kiniweka Mimi Zogwale kuwa mwanaume wa heshima hata tungeachana leo akiaga dunia nitampa treat anayostahili. Sitaona aibu kutaja ni mke wangu tulianza kupambana pamoja. After all hataweza kufufuka kusimama kama mke tena au kuziba mchepuko au mke mwingine niliye naye kwa mfano. Nimemaliza
 
Mungu atusaidie, alikuwa amempokea Yesu na ameokoka, Yesu ni mwokozi, na matajiri wengine igeni mfano wa Mengi kuokoka, hata Klyn naye anampenda Yesu
Hiyo kuokoka usiseme mengi juu ya hilo maana anaejua nani kaokoka au nani hajaokoka ni Mungu Baba mwenyewe Lakini sisi wengine tunaona ila hatuni
 
RIP mzee wetu wa nchi, pole sana kwa familia na nchi kwa ujumla.wote tu binadamu ili kuna wenye impact kubwa sana kwa nchi na watu wake.
 
Nimestushwa na kifo cha mzee mengi, ila nimestuka zaidi kuwa kafia uarabuni, niuize kwanza, kafia hotelini au hospital?

Hivi kweli weledi wote wa prof Janabi hakuweza kumpatia tiba stahiki? Mbona mzee wetu Sumayi katibiwa na prof janabi na huyo bhukheri?
 
Mkuu mbona umeripoti kirahisi hivyo taarifa ngumu namna hii?
Ni ukweli mchungu!! Kwa kilichotokea, hata mtu angezungusha vipi maneno; hatimae angefika tu kwenye kiini. Tumwombe Mungu atujalie kufikia mauti yetu tukiwa upande wake. R.I.P mzee Reginald Abraham Mengi; Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…