Mwenyekiti Simba atajwa kuwa kikwazo kwa MO

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Kumekuwa na sintofahamu ndani ya uongozi wa Simba baina ya Mwekezaji Mohammed Dewji ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa klabu ya Simba Swedi Mkwabi

Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Mo hafurahishwi na utendaji kazi wa Mkwabi ambapo amemtuhumu kuhujumu baadhi ya mipango ya klabu

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mo ameendelea kuweka jumbe tata ambazo zinaashiria kutofurahia kufanya kazi na baadhi ya viongozi wa Simba

Inaelezwa Mo ametoa masharti kuwa kati yake au Mwenyekiti, mmoja anapaswa kuondoka kwenye nafasi yake ili mambo yaendelee

[http://phpstack-189796-562565]
 
Mo hana lolote, anataka wakurugenzi mazezeta wanaomuunga mkono ili apore club for free. Nkwabi yuko pale kulinda 51% ya hisa! kimsingi ndiye anayepaswa kuwa mkurugenzi wa bodi! To hell with MO!
Ana weza kununuliwa vile vile... Ila ni mapenzi ya Mo...

Akimpa pesa Mkwabi awezi goma kuwa mjumbe ndio...

Kwenye uzia penyeza rupia... Tafakari kwa kina kaka...
 
KIKWANGO ni nini?
 
Mo hana lolote, anataka wakurugenzi mazezeta wanaomuunga mkono ili apore club for free. Nkwabi yuko pale kulinda 51% ya hisa! kimsingi ndiye anayepaswa kuwa mkurugenzi wa bodi! To hell with MO!
Inaonekana hujui chochote kuhusu biashara na uwekezaji?!! Kwa kukupa taarifa kidogo ni kwamba Simbasc upande wa wanachama,wana hisa jumla 51%lakini walizo kubaliana kwa sasa kuziingiza kwenye uwekezaji ni 11%,na mgawanyo wake uko hivi :waasisi wa club wamepewa 1%wanachama wengine ni10%.mwekezaji yeye anabaki na asilimia zake 49.ndio maana unaona kwa sasa mwenyekiti wa board ni mwekezaji maana kwa sasa yeye ndo ana hisa nyingi kwa sasa.na katika biashara ya hisa ni ngumu kupora hisa kama unavyofikilia!!unaporaje kwa mfano?!! Nafikili wengi hawaelewi biashara na uwekezaji.
 


Kama waasisi wamepewa 1% na wanachama 10% na yeye MO(mwekezaji) 49% hizo % zingene ziko wap?
 
Mo aanzishe timu yake.. fedha za kusajilia anazo.. hizi timu kongwe apa nchini zna mamb mengi.
 
Nimemdharau sana Dewji,hata kama ndiyo kuna hujuma,reaction yake mitandaoni ni ya kitoto sana. Kiongozi aliyeiva hawezi kuleta mambo ya taasisi mitandaoni
Binafsi nimeshangaa mtu kama Mo kulia lia kwenye mitandao. Ama kweli pesa sio kila kitu. Mo ana akili za kitoto na nimefikiria bila pesa za urithi asingeweza kusimama yeye kama Yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…