Mwenyekiti UVCCM asimamishwa kazi.

Mwenyekiti UVCCM asimamishwa kazi.

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, imemsimamisha kazi Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bw.Jonathan Agustino Madete ,kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.

Maamuzi ya Kikao hicho yametolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, mkoa wa Shinyanga Bw.Richard Masele.

SOURCE ITV TZ

Wakuu naomba sapoti yako kwenye andiko langu SO4C
 
Bwana Jonathan kakutwa na kosa gani la kumsimamisha kazi? Au ndio yale mambo 😂😂😂😂😂😂😂
 
Viongozi wa CCM wazidi kukengeuka

WENYEKITI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI JONATHAN MADETE ATUMBULIWA​

MaduhuJune 13, 2024

MWENYEKITI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI JONATHAN MADETE ATUMBULIWA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga,imemuachisha nafasi ya uongozi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Agustino Madete kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Richard Masele, amebainisha hayo leo Juni 13,2024 wakati akitoa taarifa ya maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho.

“Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mabala Mlolwa, kilichoketi leo, pamoja na mambo mengine kimemuachisha nafasi ya uongozi ndugu Jonathani Agustino Madete Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa sababu ya utovu wa nidhamu,”amesema Masele.

Aidha, amesema vilevile Halmashauri Kuu imeazimia kwamwe haitamfumbia Macho wala kumvumilia Mtu yeyote awe kiongozi au Mwanachama wa CCM, atakayevunja kanuni,taratibu na Katiba ya Chama hicho, kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa mara moja dhidi yake.

Amesema hiyo sababu ya kulinda heshima ya Chama na Jumuiya zake, ili kuhakikisha misingi ya Chama na miongozo inaendelea kuheshimiwa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa mheshimiwa Dr. Samia Hassan ambaye ni mahiri, mchapakazi, na mzalendo wa kweli .

Jonatha Agustino Madete aliyetumbuliwa Uenyekiti UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa madai ya utovu wa nidhamu

Source: Shinyanga Press Club Tanzania
 
Back
Top Bottom