Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohammed Ali Kawaida, amesema kupitia ushirikiano ulioanzishwa na Serikali ya Tanzania katika maeneo ya bandari, utasaidia kuondoa changamoto za gharama na ufanisi wa bandari ya Dar es salaam, unaopelekea wafanyabiashara kupitisha bidhaa zao kwa gharama kubwa au kutumia bidhaa zinazosafirishwa na nchi shindani.
Kawaida amebainisha hilo leo jijini Dar es Salaam, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa babari kuhusiana a masuala mbalimbali yaliyoainishwa katika makubaliano baina Serikali ya Tanzania na Dubai, kwa lengo la kupunguza upotoshaji unaodaiwa kufanywa na watu mbalimbali.
Mwenyekiti huyo, amesema baadhi ya maeneo ambayo yalipotoshwa ni pamoja a muda wa Mkataba husika, bandari za Tanzania kukabidhiwa kwa Serikali ya Dubai na Kampuni ya DP World, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kufa, Bandari ya Dar es Salaam kukabidhiwa kwa Serikali ya Dubai, Usalama na Ulinzi wa bandari unakabidhiwa kwa wawekezaji pamoja wazawa kupoteza ajira.
"Kwa sasa, tuko kwenye hatua ya kwanza ya Makubaliano baina ya Serikali mbili. Makubaliano hayo yana mawanda mapana sana (wide scope) ya maeneo ya mashirikiano baina ya Serikali mbili. Kufuatia Kuridhiwa kwa Azimio na Bunge, Serikali itaendelea na hatua ya pili ya kuandaa Mkataba wa Nchi Mwenyeji na baadaye Mikataba Mahususi ya Utekelezaji wa Utoaji wa Huduma, Uboreshaji, Uendelezaji na Undelezaji, kiwango cha uwekezaji kitakachowekezwa, muda wa mikataba, mapato ya TPA, vigezo na viashiria vya utendaji, wajibu wa pande mbili na masuala mengine yote mahsusi ya mkataba yatafafanuliwa.
"Naomba kutumia fursa hii kuuomba umma kupuuza upotoshaji unaofanyika kwa sababu hauna nia njema kwa Serikali, watuamiaji wa bandari zetu na wananchi wote wa Tanzania. Upotoshaji huu unalenga kudhooofisha juhudi za Serikali katika kuvutia uwekezaji, kuongeza fursa za ajira pamoja na kufungua fursa za kiuchumi zenye manufaa katika Sekta nyingi ikiwemo ya usafirishaji, uzalishaji, viwanda, afya na elimu," ameswma Kawaida.