PreGE2025 Mwenyekiti UWT Njombe asema watailinda CCM kwa gharama yoyote ile kama Simba na Yanga

PreGE2025 Mwenyekiti UWT Njombe asema watailinda CCM kwa gharama yoyote ile kama Simba na Yanga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Njombe, Dkt. Scholastika Kevela, amewataka wanawake kote mkoani humo kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza kuwa chini ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna atakayeweza kuvuruga mchakato wa uchaguzi.

Dkt. Kevela ametoa kauli hiyo wilayani Makete, wakati wa kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Njombe kilichofanyika na kuwahusisha wajumbe wa baraza la UWT Wilaya ya Makete. Katika kikao hicho, walijadili masuala mbalimbali ya ujenzi wa Jumuiya na uimarishaji wa Chama kwa ujumla.

Akijibu kauli ya baadhi ya vyama vya upinzani vinavyosema “No Reform, No Election,” Dkt. Kevela alisema:

“No reform no election anakimbia na mpira kwapani... hiki ni Chama Cha Mapinduzi na uchaguzi utafanyika, yani iwe mvua au jua, uchaguzi upo.”

Amesisitiza kuwa wanawake wa CCM wamejipanga kuhakikisha wanakilinda Chama chao kwa gharama yoyote ile, na kwamba hakuna nafasi ya hofu wala sintofahamu kuhusu mustakabali wa uchaguzi.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Mkoa wa Njombe, Aziza Kiduda, amewahamasisha viongozi wa Jumuiya kuongeza juhudi katika ujenzi wa nyumba za UWT na kuwekeza katika miradi ya kiuchumi ambayo itaifanya Jumuiya kuwa imara zaidi na yenye uwezo wa kujitegemea.

 
tushawazoea mpaka kuteka si kazi zenu CCM
 
Back
Top Bottom