Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MWENYEKITI WA UWT TAIFA AONGOZA KONGAMANO LA MAFUNZO YA MATOKEO YA SENSA, KAHAMA, SHINYANGA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Marry Pius Chatanda ameongoza Kongamano la Mafunzo ya Matokeo ya Sensa kwa Makundi mbalimbali lililofanyika Julai 1,2024.
Kongamano hilo liliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba lililofanyika Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kutoa Mwelekeo wa CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu.
Mbunge Santiel amesema kuwa Kongamano hilo limejumuisha viongozi wa CCM na Serikali wakiwemo Wakurungezi wote wa Halmashauri (Shinyanga), Wabunge, Watendaji, Mama Lishe, Wajasiriamali, Waponda Kokoto, Walimu, Manesi, Maaskari, Watu wenye ulemavu.