Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Maalim Seif kuzungumza na vyombo vya habari kesho

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kesho Oktoba 20, 2020 atazungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Wapi: Ukumbi wa Ramada Hotel, jirani na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Posta Mpya, Dar es Salaam.

Muda: Mkutano huo utafanyika saa 4:00 asubuhi

Baada ya mkutano huo, Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Zanzibar atahutubia mkutano wa hadhara Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Barafu Mburahati, Ubungo.

Aidha Maalim Seif atatumia mkutano huo kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wote wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam.

Waandishi wa habari kama wadau muhimu mnakaribishwa katika matukio hayo.

Imetolewa na:

Janeth Joel Rithe

Naibu/Katibu wa Uenezi, Habari na Mahusiano ya Umma

Leo Oktoba 19/10/2020

 

Attachments

Na imani na Maalimu na suala la Membe litatolewa ufafanuzi
 
CCM inapigwa kotekote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…