The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Kutoka kwenye viunga vya lango la kuingilia Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam mvutano umeibuka baina ya maafisa wa Jeshi la Polisi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao leo, Jumatatu Septemba 15.2025 wamejitokeza kwa wingi Mahakamani hapo kuja kusikiliza uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili.