Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI akutana na Menejimenti

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI akutana na Menejimenti

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Dkt. Marina Njelekela ametembea taasisi hiyo na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Menejimenti ambapo amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Njelekela ametembelea MOI leo Mei, 21, 2025 ambapo amesema lengo la kukutana na wajumbe hao wa menejimenti ni kupata taarifa za awali za majukumu ya kurugenzi na vitengo vyao, mafanikio na changamoto ili kujenga uelewa wa pamoja juu ya taasisi hiyo.

“Nimefurahi kukutana na wajumbe wa menejimenti na kupata taarifa za majukumu, utekelezaji na changamoto za kurugenzi na vitengo wanavyoongoza ... taarifa hizi za awali zitanijenga mimi kama mwenyekiti kuifahamu kwa kina taasisi yetu” amesema Mwenyekiti huyo na kuongeza

“Niliona bora nije ili tufahamiane ana kwa ana na wajumbe, ningeweza kuitisha taarifa nikaisoma ila nikasema bora tuonane ili nipate muda kwa kuwasikiliza na kujadiliana mambo mawili matatu”

Kwa upande wake MKurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amemkaribisha mwenyekiti huyo wa bodi ya wadhamini ya MOI na kuahidi kushirikiana naye katika kuiendeleza taasisi hiyo kwa maslahi ya wananchi.

“Karibu sana mwenyekiti, nikupongeze kwa uteuzi wako na nikuahidi kuwa mimi na wajumbe wa menejimenti tuko tayari kushirikiana na wewe katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora za matibabu ya kibingwa na kibobezi” amesema Dkt. Mpoki

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa mwenyekiti huyo wa bodi ya wadhamini wa MOI tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania Mhe😀kt. Samia Suluhu Hassan Machi, 12, 2025.
IMG-20250521-WA0109.jpg
IMG-20250521-WA0094.jpg
IMG-20250521-WA0091.jpg
IMG-20250521-WA0097.jpg
IMG-20250521-WA0089.jpg
IMG-20250521-WA0104.jpg
 
Back
Top Bottom