Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa amesema kitendo cha aliyekuwa Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwataka Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya hakikuwa sahihi, kwani tayari ilani ya uchaguzi ya chama hicho ilishaahidi kushughulikia suala hilo.
Mlolwa amesema hayo Septemba 2, 2026 alipokuwa akizungumza na wanachama hao eneo la Kishapu mkoani Shinyanga ambapo amedai kuwa pamoja na kuwa ilani imeshasema juu ya hilo na Nchimbi alishiriki kuinadi, tayari alikuwa ni mshauri namba moja wa Rais na angeweza kuzungumza na Rais Dkt. Samia moja kwa moja juu ya jambo hilo.
Julai 24, 2026 Dkt. Nchimbi akizungumza na watetezi wa haki za binadamu Mlimani City alisema kama angekuwa na nafasi moja ya mwisho kuzungumza na watanzania angewataka kupambania mpya huku akidai kuwa Rais tayari ana nia ya dhati ya kuipata katiba hiyo hivyo watanzania washikilie jambo hil