- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu salaam, Naomba msaada juu ya uhalisia wa taarifa hii inayosambaa mtandaoni kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ni mahututi na amepelekwa Afrika kusini kwa ajili ya matibabu.
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye alikuwa ni moja kati ya waasisi wa chama hicho mwaka 1992 na mwaka 2005 alikuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya CHADEMA, lakini pia mwaka 2010 hadi 2020 alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mwaka.
Mnamo Oktoba mosi 2024, Freeman Mbowe alihudhuria katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mahakama hiyo ilitegemewa kutoa uamuzi mdogo juu ya dhamana ya Boniface Jacob, ambaye hivi karibuni ameshinda uenyekiti Kanda ya Pwani ndani ya CHADEMA.
Kumekuwepo na taarifa inayosambaa mtandaoni ikieleza kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe yupo katika hali mahututi na amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
Je uhalisia wa taarifa hii ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia vyanzo vya kuaminika umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haijatolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Aidha Mkurugenzi wa ltifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X amekanusha juu ya uwepo wa taarifa hiyo akiwataka watu kuipuuza kwani ni uzushi na haina ukweli wowote.
Kadhalika mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya kaskazini Godbless Lema ameikanusha taarifa hiyo kuwa si ya kweli na kwamba ipuuzwe kwani Freeman Mbowe yupo nyumbani kwake Machame wakipanga mipango ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.