Sijui kwa nini, yaani tangu juzi nina amani sana rohoni; Kuhusu mama yetu kuwa Rais yaani roho yangu imefarijika mno - sijui ninyi wenzangu huko mnajisikiaje.
Ninachokiomba tu kwa Mwenyezi Mungu amtie nguvu kubwa na ujasiri mkubwa huyu mama ili hao CCM wasithubutu kumharibu - asimamie msingi ya utawala bora ili vizazi na hata vizazi vijavyo vimkumbuke kama Mwanamke Rais Jembe kuwahi kuliongoza Taifa letu.
Hongnera sana mama yetu !! Ingawa naiona kazi kubwa mno iliyopo mbele yako ya kuliungaisha Taifa letu kwa Upendo, Umoja na Mshikamano kama lilivyoachwa na baba wa Taifa.... haya ma vyama yetu haya yasiwe uwanja wa vita, chuki na umwagaji wa damu - komesha kabisa ndani ya utawala wako.
Salute !!