"---ila aache kung'ang'ania uenyekiti,----".
Inawezekana ukawa sawa, kama wewe ni mgeni Tanzania.
Je, inawezekana uwepo wa CHADEMA, kama ilivyo sasa, katika hali ngumu kabisa iliyokikabiri chama katika miaka mitano iliyopita huenda ingekuwa ni tofauti kabisa na iliyopo sasa?
Hili ni swali tu, hata wewe unaweza kujiuliza na kulijibu kivyako!
Mimi nadhani CHADEMA, kama ingebahatika kuendelea kuwepo kama chama, hali yao ingekuwa ni tofauti sana chini ya uongozi wa mtu mwingine mbali ya Mbowe.
Usinielewe vibaya. Sisemi kamwe kwamba hakuna viongozi wengine ndani ya CHADEMA, ambao pengine ni imara zaidi na hata kuwa bora zaidi ya Mbowe; lakini wakati CHADEMA ilipopata dhoruba kali, ilibahatika sana kuwepo na Kiongozi imara kama Mbowe.
Bila shaka, kama dhoruba lile litakuwa limepita, inawezekana sasa hata Mbowe mwenyewe na chama chake wakawazia jambo la kupata uongozi mpya.
Huo utakuwa ni uamzi wa wanachama wao, na sio shurti kutoka nje.