Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Wilbard mashauri mjinga anaendekeza tumbo lake hana reference ya kisheria sasa kawa jaji ndio aendelee kutunisha mtumbo wake kwa tamaa ya madaraka mpuuzi kabisa Mungu amlaani yeye na kizazi chake
Malipo yake yanakuja , Kama Mbwai na iwe Mbwai
 
mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi “ - Jaji Rumanyika

“ hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri Lakini Wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi “ - Jaji Rumanyia

“ ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi “ - Jaji Rumanyika

“ Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia HAKI “- Jaji Sam Rumanyika .

Chanzo:Ukurasa wa twitter wa Zitto
 
Inasikitisha sana huyo laanatu anavyoingilia uhuru wa mahakama na watu wanawekwa ndani miezi chungu nzima kinyume cha sheria lakini hakuna yeyote anayeadhibiwa.

BREAKING NEWS .....
Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masikini ya Mungu pesa za matibabu na school fees za wanawe tumeona clip anaomba kwa diaspora huko US sasa pesa za kununua nafasi ya kugombea urais atazitoa wapi? Unafikiri Wachagga watampa bure hiyo nafasi?
Masikin ni wew pamoja na mama yako.
 
Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.

1. Kesi inadhaminika
2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.
3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana
4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana
5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.
6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.
7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani
8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani
9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.

Tanzania bado Ina majaji kwa hakika. Mola ampe maisha marefu Jaji Sam Rumanyika

Zitto Kabwe
7/3/2019
 
Hujui kama Lissu katangaza kugombea urais?
Kumbe na wewe AKILI MATOPE? Lissu kasema kwamba kama atapendekezwa na chama chake, yupo tayari kugombea Urais. KUTANGAZA KUGOMBEA URAIS ni ishu nyingine kabisa
 
Mlaanifu azidi kulaaniwa na Mwenyezi Mungu kwa kupindisha sheria za nchi ili kukomoa Watanzania.

Back
Top Bottom