Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Ukisikia unafiki uko sura nyingi alikuwa wapi kusema kabla
 
Watawala wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu badala ya kuendelea kutenda dhambi kwa kuomba waombewe wakati wakijua fika kuwa matendo yao ni kiuonevu dhidi ya RAIA walioapa kuwalinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
========

UPDATE:



Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama Kuu jijini Dar‬


Maneno ya Jaji Rumanyika akisoma hukumu

Mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi. Hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri lakini wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi

Ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi.

Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki.

=====


Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba. Mahakama yaagiza warufani waachiwe mara moja.

Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika

2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.

3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana

4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana

5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.

6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.

7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani

8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani

9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.

Halafu yule hakimu aliyefuta dhamana ya mbowe na ester ndio kwanza jiwe kampandisha cheo kwa kazi nzuri aliyomfanyia kuwakomesha wapinzani ukisoma maelezo ya jaji was mahakama kuu utaona kabisa jamaa hana sifa ya kuwa hata hakimu wa kata halafu kabudi anasema nchi inaendeshwa kidemokrasia tuwache utani .
 
Nilikua mahakamani kwenye kesi nyingine hukumu ya Mbowe na Esther ilivyo toka: tulisikia furaha za watu mpaka kwenye Chamber za Majaji. #Ruleoflaw
Hata sisi CCM tulisikia furaha mno kuwa kweli mahakama iko huru na inatenda haki tofauti na wengine wanaosema mahakama haiko huru na haitendi haki .tumelipuka kwa furaha sana hongera sana chadema kwa ushindi mnono .
 
Faiza ulikosa uteuz enzi za jk,wenzako wote waliokua wamejaaliwa neema za Allah kama ww ulivyo na tako kubwa walilamba uteuzi udc awamu hii unajipendekeza kwa kasi unatamani mpaka kuingia kanisani lkn hawakuoni tu pole sana

Ha haaaaaa , huyu Bibi leo kashindwa kuchangia mpaka nime hisi Wadukuzi wanacheza na ID yake😂😂..
 
Amini nawaambia Mzee Meko atafanya uteuzi weekend hii ili apate nafasi ya kuapisha na kutoa hotuba ya kumshambulia huyu Jaji na Muhimili wa Mahakama kwa ujumla.... stay tuned
 
Back
Top Bottom