Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

Hata sisi CCM tulisikia furaha mno kuwa kweli mahakama iko huru na inatenda haki tofauti na wengine wanaosema mahakama haiko huru na haitendi haki .tumelipuka kwa furaha sana hongera sana chadema kwa ushindi mnono .
Shida ya Ako Kamama Ni Kaongo na Kasahurifu, Leo Prof. Judge Rumanyika Angekuja Na Maamuzi Tofauti Wala Asingeandika Aya Yote, Wanasiasa Wajifunze Akili Zao Kuwa na Akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana pia waliamua tu kuwaweka ndani
Kila mtu alisema humu kuwa basi wamuachie imetosha ila wanataka kujionyesha wamefanya kazi kubwaaa kumbe watu wameamua tu kuwatoa

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Mataifa mengi yanazalisha waasi kwa mtindo huu wa kunyimwa au kuchelewesha kutoa haki za msingi na za kikatiba. Pole sana Mh Matiko na Mbowe, pole sana viongozi wa upinzani. Nilichojifunza kwenu nikuwa ninyi ni wazalendo na wapenda amani kuliko yoyote katika nchi. Inatosha ktk Mateso haya ninyi kuhamua lolote sasa...
 
Kuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!

Hii leo atalala fofofo!

Hii leo atawasimlia wakeze!

Hii leo hataisahau kamwe!

Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!

Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!

Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.

Haya sasa jifanye unaumwa tena.

Povu ruksa!
 
Mbona jiwe anaelekea huko!
 
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
========

UPDATE:

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama Kuu jijini Dar‬

Maneno ya Jaji Rumanyika akisoma hukumu

Mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi. Hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri lakini wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi

Ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi.

Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki.

=====

Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba. Mahakama yaagiza warufani waachiwe mara moja.

Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika

2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.

3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana

4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana

5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.

6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.

7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani

8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani

9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.

Hakika ni uamuzi wa kihistoria katika dhana ya kuondoa unonevu wa kisiasa ndani ya mahakama zetu.
Mahahama zote zikiwa na mtizamo wa kikatiba kama wa Jaji Rumanyika haki itakuwa inaonekana kwa uwazi zaidi na dhana ya uhuru wa mahakama kutoingiliwa itakuwa dhahiri
 
Sasa hivi akiambiwa tarehe ya kesi yake anaweza kwenda siku mbili kabla kwenda kusubiria hapo hapo mahakamani. Najua ameielewa mahakama sasa sio kule wanakopiga kelele ' MONGOZO!!! ' MONGOZO!!! Mwisho wa siku wanatolewa tuu nje mambo yanaishia hapo.
 
Kuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!

Hii leo atalala fofofo!

Hii leo atawasimlia wakeze!

Hii leo hataisahau kamwe!

Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!

Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!

Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.

Haya sasa jifanye unaumwa tena.

Povu ruksa!
Shut up we mkolomije
 
Nahisi Mbowe na matiako watakuwa wametia akili kwa sasa. Wamwache aje kupambana na Lissu.
Kumbe hoja ilikuwa kumtumia hakimu wa mahakama ya Kisutu kuwashikisha adabu.
Siamini kama haya yanasemwa na mwelevu Faizal
 
Watu kama ninyi ndio ambao wakati ule wa utumwa mlikuwa hamtaki kupinga lolote kutoka kwa waarabu, hata wakihitaji mlikuwa tayari ili tu muishi vizuri.
Sehemu ya MAPAMBIO kama mliyokuwa mnamwimbia Jeuri yule.
 
Back
Top Bottom