Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa iyo unamfananisha mandela na bwana mawani!!!Hata Mandela aliteswa na makaburu lakini leo hii dunia nzima inamthamini kuliko hata hao makaburu walioijenga South Africa.
Mwanasiasa anakuwa na roho mbaya kama shetani halafu unataka watanzania tukuombee, huo ni uroho na ulafi wa maombi
Haiondoi uhalisia kwamba jamaa kaadabishwa kweli kweli!
Nahisi Mbowe na matiako watakuwa wametia akili kwa sasa. Wamwache aje kupambana na Lissu.
Dhamana ya jaji iliwataka watoe taarifa kila wiki polisi. Nayo ni uccm au haki?Jaji katenda haki kabisa nakubaliana na uamuzi wake wenye hoja zilizoshiba . Mahakama imeonyesha wazi jinsi ilivyo huru kufanya maamuzi na hukumu na jinsi inavyotoa haki bila woga wala upendeleo.Hongereni Mbowe na Matiko kwa ushindi mnono mliopata mahakamani.Na hongereni mahakama kwa kutenda haki
Hatari!
Sheria za kiharusi umefutika kwenye makalio?Mandela wa ufipa katoka ngoja tusubirie cheche zake, ila hatarudia tena kuidharau mahakama.
Tunaomba wataalam wa sheria mkazie hii hukumu ili iwe na manufaa kwa wengi mpaka maccm yasiyojielewa maana yenyewe ndio majizi yako mengi ili wasikose haki ya dhamana, na ule mtindo wa wadhamini wawili lazima wawe wafanyakazi wa serikali ni batili na kinyume cha katiba, serikali imeajiri watu wangapi miongoni mwa Watanzania millioni 50?Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
========
UPDATE:
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama Kuu jijini Dar
Maneno ya Jaji Rumanyika akisoma hukumu
Mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi. Hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri lakini wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi
Ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi.
Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki.
=====
Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba. Mahakama yaagiza warufani waachiwe mara moja.
Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika
2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.
3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana
4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana
5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.
6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.
7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani
8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani
9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.
Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.
kwa utawala huu yatakufika Tu,Kuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!
Hii leo atalala fofofo!
Hii leo atawasimlia wakeze!
Hii leo hataisahau kamwe!
Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!
Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!
Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.
Haya sasa jifanye unaumwa tena.
Povu ruksa!
Kwa iyo wew unaona walikuwa wanaonewa!?Kumbe majitu bado matoto namna hii?
Jitu zima lina mvi mpaka matakoni lipo JF linashangilia uonevu usio na maana?
Tuna safari ndefu sana!
Mandela hakuwa mkwepa kodi...Hata Mandela aliteswa na makaburu lakini leo hii dunia nzima inamthamini kuliko hata hao makaburu walioijenga South Africa.
Nikiwa jeuri kama yeye acha na yanifike.kwa utawala huu yatakufika Tu,
WEwe ndio unapata shida yeye wala hana shidaKuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!
Hii leo atalala fofofo!
Hii leo atawasimlia wakeze!
Hii leo hataisahau kamwe!
Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!
Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!
Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.
Haya sasa jifanye unaumwa tena.
Povu ruksa!
Huyu ni Baba Keagan
Mimi nilikacha misa ya jana kwa vile kwenye kanisa ninalosali waliingia watu ambao si wa Mungu , siwezi kushiriki ibada moja na mawakala wa shetani wanaojulikana waziwazi