Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,797
- 28,904
Hii nchi lazima ikombolewe kutoķa kwa wahuni SISIEMU
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatarudia tena.Sheria za kiharusi umefutika kwenye makalio?
Bavicha mna mattz ya akili sio bure, hivi mtu kakaa miezi mitatu huko ndani leo unasema aibu kwa mashauri, Nani kaumia kati ya Mbowe na mashauri?Ni aibu kubwa sana kwa Jaji Mkuu na ni aibu kubwa sana kwa Wilbard Mashauri na familia yake
Kwani yeye ni mhalifu? Kesi za kubambikiza zinaelekea ukingoni.Hatarudia tena.
Kwenda zako... sasa mmefaidika nini zaidi.... Ya kuongezachuki. Kati ya serekali na raia? Kila chenye mwanzo kina mwisho. Hata hii serekali dhalimu ina mwisho wake.Hatarudia tena.
Wewe wa kwanza kuumia.Bavicha mna mattz ya akili sio bure, hivi mtu kakaa miezi mitatu huko ndani leo unasema aibu kwa mashauri, Nani kaumia kati ya Mbowe na mashauri?
The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Hapana yeye ni mtuhumiwa tu ndio maana anayo haki ya dhamana, na mahakama imempatia.Kwani yeye ni mhalifu? Kesi za kubambiza zinaelekea ukingoni.
Mashauri ajiandae kulipa gharama , Mungu hajawahi kuwa falaBavicha mna mattz ya akili sio bure, hivi mtu kakaa miezi mitatu huko ndani leo unasema aibu kwa mashauri, Nani kaumia kati ya Mbowe na mashauri?
The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Tattizo ni uelewa wa ufipa tu, ila kuruka dhamana ni kosa ambalo linakufutia dhamana yenyewe, ni taratibu tu za kisheria jinsi zilivyo, hakuna mtu mwenye chuki na mtu kamanda.Kwenda zako... sasa mmefaidika nini said I. Ya kuongezachuki. Kati ya serekali na raia?
Sheria gani walikiuka ambazo jaji Rumanyika hajaziona.Unaongea ujinga gani? Fidia ya nini kwa kukiuka sheria ya dhamana? Kwanza inabidi waishukuru mahakama kuu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Don't say that! We need people like him.Jaji mkuu anapaswa kujiuzulu haraka sana .
Mwenzenu huyoKuna haja kanisa katoliki liwe linawanyima komunyo watesaji wa binadamu wengine Bila makosa?
Fikiria mbowe amelia ndani kwa miezi nitatuma lkn Mzee anakunya damu ya yesu,na Kula mwili wa yesu Kila jumapili Bila kizuizi
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna wapuuzi wanampa maneno ya faraja mara oo Mandela wa Tz mara oo kesho ni nzuri kuliko jana-ujinga!Kwa taarifa yenu cha moto amekipata!
Hii leo atalala fofofo!
Hii leo atawasimlia wakeze!
Hii leo hataisahau kamwe!
Huwezi kukaidi Mamlaka na ukabakia ukichekewa tu kama mtoto mrembo.Huwezi kujifanya unayo akili na utafanya kile ukitakacho bila kuwa na adabu!Cha moto ame.....!
Haya tena jifanye kujifaragua ili wakufarague tena.Miezi mitatu kile kiugonjwa kilienda wapi vile!?hahahahahaha!
Mamlaka ni Mamlaka bwana makengeza na inao uwezo wa kukufanya itakavyo na hutafanya lolote!Zaidi utaimbiwa vimapambio kama walivyokuwa wakikuimbia.
Haya sasa jifanye unaumwa tena.
Povu ruksa!
Umesoma hukumu ya jaji we kenge?Kuna mahali imeonesha km asirudie kuidharau mahakama?Hii ni tafsir ya mashaur na jiweMandela wa ufipa katoka ngoja tusubirie cheche zake, ila hatarudia tena kuidharau mahakama.
Nahisi Mbowe na matiako watakuwa wametia akili kwa sasa. Wamwache aje kupambana na Lissu.
1. Kesi inadhaminikaDaah kule Si kuzuri kabisa, jambo la heri kama wametoka,ila ni vema wasirudie kosa kama hilo la kuidharau mahakama
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
========
UPDATE:
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko wameachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana katika Mahakama Kuu jijini Dar
Maneno ya Jaji Rumanyika akisoma hukumu
Mahakama ya Kisutu ilikabidhi jukumu lake kwa Polisi. Hakuna mahala popote warufani wamezuiwa kusafiri lakini wakati huo huo wanatakiwa kuripoti Polisi kila Juma. Hii maana yake wamenyimwa Uhuru wa kusafiri na haki ya kufanya kazi
Ni hatari sana kunyima dhamana mtu bila sababu za Msingi.
Hii ni rufaa mojawapo sijawahi kuiona Katika kazi yangu ya Ujaji. Maofisa wa mahakama kama mahakimu wanapaswa kutumia utashi wao kuamua haki za watu kwa kuzingatia Haki.
=====
Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam chini ya Jaji Rumanyika yatengua uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu wa kufuta dhamana za Mhe Freeman Mbowe na Mhe Esther Matiko. Mahakama hiyo imeeleza kusikitishwa na ufutaji wa dhamana hizo na kuzitaka mahakama za chini zijionye kabla ya kufikia maamuzi yasio ya haki na kikatiba. Mahakama yaagiza warufani waachiwe mara moja.
Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.
1. Kesi inadhaminika
2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.
3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana
4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana
5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.
6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.
7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani
8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani
9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.
Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.