Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew amehamia CCM na kueleza kuwa amerudi nyumbani. Amesema kuwa amerudi CCM kuunga mkono juhudu za maendeleo zinazoletwa na chama hicho.
Erythrocite
JF-Expert Member
Sakata la Nape la kuomba radhi kwa Mwenyekiti wa ccm limeambata na vitisho vya kuvuliwa ubunge na chama chake , kisha ubunge huo kukabidhiwa ndugu Suleiman Methew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi , taarifa zinadokeza kwamba Philipo Mangula naye ameingia kwenye siasa za kishamba za kununua watu , ambapo aliingia makubaliano na Methew ya kurejea CCM, chama kilichomtosa kwenye kura za maoni 2015 na baadaye kumfunga Jela , aliokotwa na CHADEMA na kupewa nafasi ya kugombea ubunge ambapo alishindwa kwa bao la mkono , hata jela alikofungwa kwa maelekezo ya ccm alitolewa na CHADEMA baada ya kukata rufaa kwa kutumia kikosi chake kizito cha wanasheria kilichoongozwa na Mh Tundu LissuNi vema Suleiman Methew mwenyewe ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ajitokeze hadharani na kunyoosha maelezo .
Nakala : Yericko Nyerere