Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini, Suleiman Mathew ahamia CCM

Erythrocite​

JF-Expert Member​

Sakata la Nape la kuomba radhi kwa Mwenyekiti wa ccm limeambata na vitisho vya kuvuliwa ubunge na chama chake , kisha ubunge huo kukabidhiwa ndugu Suleiman Methew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi , taarifa zinadokeza kwamba Philipo Mangula naye ameingia kwenye siasa za kishamba za kununua watu , ambapo aliingia makubaliano na Methew ya kurejea CCM, chama kilichomtosa kwenye kura za maoni 2015 na baadaye kumfunga Jela , aliokotwa na CHADEMA na kupewa nafasi ya kugombea ubunge ambapo alishindwa kwa bao la mkono , hata jela alikofungwa kwa maelekezo ya ccm alitolewa na CHADEMA baada ya kukata rufaa kwa kutumia kikosi chake kizito cha wanasheria kilichoongozwa na Mh Tundu Lissu

Ni vema Suleiman Methew mwenyewe ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ajitokeze hadharani na kunyoosha maelezo .

Nakala : Yericko Nyerere
 
Sawa
 
Tuna wanasiasa wanao-fit sifa za wanyama hawa kuliko hata
Tulia wewe hujajua siasa bado endelea kujifunza
Wenzio wameshafungwa na kupoteza kila kitu shauri ya chadema,wewe unajificha ficha nyuma ya keyboard
Siku utakayopangwa mstari wa mbele halafu chama chako kikakupuuza utaelewa kwa nini wengine wameamua kurudi ccm
 
Kila nikisikia kuna mtu kaihama chadema ndivyo ninavyozidi kuipenda na sitaacha kuipenda chadema my heartly loved political part
 
Mbona unaweweseka Dada anguuu?
 
Mama anaendeleza mema yote ya Magufuli kwenye chama na serikali.
Wembe ni uleule.
 
Maana sidhani kama akina He tunakimbiaga mapambano aisee!

Anashindwa kujua msimu huu wa Samia ni wrong move kuhamia CCM maana CCM original ndio wameshika chama chao,sio enzi za hayati Mungu!
Kwa hiyo Lisu ni mwanamke? Maana nae si kakimbia mapambano?

Alafu wewe huwezi kumjua huyo jamaa maana wewe siyo mwanasiasa ila ni shabiki tu
 
Ni kama hesabu za cross multiplication.

Mahasimu wa jadi Nape Nnauye na Suleiman Methew wamekubaliana yaishe na sasa wanasukuma gurudumu moja la maendeleo.

Kazi Iendelee!
 
Hakuna atakayebaki chadema
Wembe ni uleule
 
kifo cha Magufuli kina utata, hata kama Mama hataki kisemwe ila yanayoelendelea yana ukakasi.

Membe alihama ACT Mwezi wa Kwanza kujiandaa na Kurejea CCM, ila target yao ni 2022
 
Mkuu, tatizo una hasira na matusi na hii tabia huwa wanayo watu wenye msongo wa mawazo!

Lisu kakimbia mapambano, hilo siyo ka kukataa!

Nyarandu alipohamia chadema mlisema hawezi kukaa na dikteta sasa kwanini yeye hukumuita mwanamke kwa kukimbia.? Kwanini hakubaki apambane ndani ya chama?
 
Mama anaendeleza mema yote ya Magufuli kwenye chama na serikali.
Wembe ni uleule.
Wakati CDM wanaendeleza siasa za kumchafua mwendazake wenzao CCM wanaendelea kukijenga chama na kuwachukulia wanachama wakongwe. Je hapo watamlaumu Magu kununua viongozi wao? CDM wabadilike wasicheze ngoma ya ccm ikulu wataisikia kwenye bomba. Na safari hii ya Samia mbinu za kuwanyoosha CDM zitaenda kisayansi zaidi.
 
Mkuu kwani kuna ubaya mtu akitumia haki yake kikatiba kuamua kwenda upande wowote......??

Nadhani hii ndio demokrasia inayopiganiwa na wanaharakati.........na moja ya nguzo zinazoshikilia demokrasia ni UVUMILIVU.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…