TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
RIP Kiukweli tunakokwenda Watanzania si pazuri kwani siasa hazipaswi kuuwana na kutufanya kuwa maadui kiasi hiki.Kila aliyeshiriki serekali isimfumbie macho imchukulie hatu kali bila kujali anatoka chama gani.
 
Labda nikuulize ni tukio la ngapi kwa wapinzani wa CCM hasa wanachama na viongozi wa CHADEMA kuumizwa na kuuawa? kama ni uvumilivu kwa sasa unatosha kwani CCM wametunyanyasa vya kutosha na isitoshe hadi wametunyang'anya ushindi wa Ubunge, Udiwani maeneo mengi bila kusahau nafasi ya URAIS, kwa sasa nafikiri inatosa kwa yeyote mwenye uwezo wa kutenda lililo jema kwa kulipa kwa alichofanyiwa ALPHONSE MAWAZO(R.IP) na afanye hivyo ili kulipia damu hii isiende bure kwani polisi hawapo tayari kutetea wapinzani wao wanaitetea CCM tu hivyo wapinzani tujilinde na kujitetea wenyewe OVER!!!
 

Tanzia Ipo Jf Kitambo Tu Mkuu
 
Alphonse Mawazo ameuawa!! Ni kijana sana;mke,watoto wake,chama chake,h?ta Taifa bado linamhitaji. Ni uhuni tu,ulafi wa madaraka ndo chanzo cha kifo cha Alphonse. Mke wake,watoto wake,wazazi,ndugu wanalia. Mimi nauliza,nami pia nilie kwa kifo cha Mawazo? Nasema hapana,sitalia, kwa nini nilie kwa tendo la kiharamia lililotendwa na wahuni? Natakiwa nimuenzi Mawazo kwa namba fulani,si kwa kulia.
IMETOSHA!!!
 
du! mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, amen! inahuzunisha sana makamanda wanapopoteza maisha kikatili kweli nchi hii haina amani kweli, kaz ipo kuelekea tanzania halisi
 
Alikuwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea udiwani katoro, ndipo walipotokea vijana wa ccm wakawazidi nguvu red bregedia na kumpiga kamanda huyu mawazo
Wakawazidi nguvu kwani walikuwa wanapigana na chanzo cha wao kupigana ni nini.
 
Siasa za kishenzi sana hizi kama kweli amekufa kwenye mambo ya siasa.
 

great words comrade
 
hapa ndio watanzania wajue ccm ni chui aliyejivika ngozi ya kondooo.na utamkuta mtanzania akijigamba kua yeye ni ccm.kama tumefikia hapa tunauana wenyewe kwasababutu ya uchama inamaana gani?nini maana ya siasa?mutashangaa. hawatachukuliwa hatua yoyote.ccm na wanachama wake niwakulaaniwa.
 
Subirini Polisi wafanye uchaguzi wao, isijekua papuch imehusika hapa siye tutapiga siasa.
 
Ukitaka kujua CCM ni wataalamu wakuwagawa watanzania tazama wanavyoraruana kwenye kugombea uspika ndani ya ccm.

Wana vita kubwa sana lkn wakishatoka nje wanajifanya wako pamoja lkn kwa uhalisia wana vita kubwa mno
 
mungu amlaze mahari pema peponi mbele yake nyuma yetu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…