Wakati wa uchaguzi wa Kanda ya Nyasa, Lissu alisema kuwa Abduli amepenyeza pesa nyingi ili mtu wake ashinde. Baada ya kushindwa uchaguzi, mtu aliyekuwa anampigia debe akatimkia kwa mama yake Abduli. Sasa ni nani alikuwa anapenyezewa hizo pesa za Abduli? Na huyo huyo ndie alikuwa anapigiwa debe na Rose! Hii ni gaslighting ya hali ya juu. Katika hili, alitakiwa achukue video au hata picha za hayo matukio ili azitumie kama ushahidi. Au atuambie alichukua hatua gani na nani walikuwa wanatoa hizo rushwa.
Hawa wanatumia falsafa ya Goebbels aliyesema " Make the lie big, make it simple, keep saying it and eventually they will believe it". Na ukitaka uaminike zaidi, ijenge kwenye kaukweli kadogo. Hapa kwetu hamna uchaguzi ( hata wa monita wa chekechea ) ambao hauna tuhuma za rushwa. Ndio maana ukitaja rushwa unaaminika kwa sababu ipo katika kila uchaguzi na watanzania wameikubali hali hio.
Amandla...