Fanfa
JF-Expert Member
- Sep 25, 2009
- 2,399
- 3,775
Ni dhahiri mwenyekiti wa Chama ukilazimisha kwa hali ilivyo hutatoboa kwenye uchaguzi ujao pamoja na kwamba wewe ndo kiongozi wa nchi.
Itakuwa ngumu wewe kujua maana hutakuwa na muda sababu utakuwa na stress za kampeni. Sababu kuu ni kwamba sasa adui yuko chumbani kwako siyo sebuleni tena. Unalala naye kitanda kimoja na bafuni mnaoga naye pamoja.
Nini cha kufanya ili kuwapiga bao au kwa lugha ya kihuni upige msamba.??
1. Kwa kuwa ndani ya chama na wao sasa wanaimba wimbo wa Reforms kama wanavyoimba wapinzani wako walioko kolokoloni na nje ya kolokoloni zenye lengo la kukuondoa kwenye game. Kubaliana nao. Na utamke wazi kuwa hoja zao zina mashiko na umekubaliana nao kwa asilimia 100.
2. Tangaza kusitisha uchaguzi mpaka hapo taifa litakapo fanya Reforms zinazopigiwa kelele na watu wa nje na ndani ya chama chako. Wewe nenda mbele yao kwa kusema minimum Reforms hazitoshi kuondoa makelele haya bali unataka full Reforms.
3. Tangaza kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya mara moja kabla ya uchaguzi wowote kufanyika. Na kwamba pesa uliyotengwa kwa ajili ya uchaguzi itatumika kufanya mchakato wa Katiba mpya.
4. Mwezi wa nane usivunje bunge badala yake extend kwa miaka miwili ili kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya na kutungwa kwa sheria na kanuni mpya zinazoendana na Katiba mpya. Hapa utaratibu ufuatwe wa kuliongezea bunge muda.
5. Itisha Bunge na kupeleka mswada haraka wa mabadiriko ya Katiba kama utaona sheria iliyopo ya mabadiriko ya katiba haikidhi haja.
6. Ikifika October ambapo ndo mwisho wa ufalme wako kikatiba, basi Peleka mswada bungeni ili yafanywe mabadiriko madogo ya Katiba kukuhalalisha uendelee kuwa mfalme hadi Katiba mpya pamoja na sheria na kanuni mpya zitapokamilika kwenye maeneo mahususi yanayoendana na uchaguzi.
7. Kwenye mchakato wa Katiba mpya, hakikisha wahuni hawachakachui tena kama walivyofanya huko nyuma. Simama na maoni ya wananchi siyo maoni ya machawa na makunguni wa ndani ya chama chako
8. Mwepuke sana yule mzee wa Msoga county. Yeye ana malengo yake ya familia siyo ya ki nchi. Usidhani kuwa anakusaidia la hasha. Mwepuke na umwogope kama Ukoma.
9. Mchakato wa Katiba ukikamilika tangaza kutogombea kiti cha ufalme.
10. Ruhusu chama chako kijihuishe upya kama wanavyodani kuwa baada ya miaka 10 chama kinajivua gamba. Wanaruhusu wafanye Reforms za ndani ya chama.
Ukifanya haya utakuwa na uhakika wa kutawala miaka miwili ijayo na pengine ikaenda hadi mitatu hivi.
Utakuwa umewapiga chenga wahuni wote na utakuwa umejijengea heshima kubwa katika taifa lako na kwa mataifa mengine yanayopiga kelele. Wananchi wako watakupenda sana, wapinzani wako watakupenda sana na wanaopenda taifa lao watakupenda sana.
Ukiupuuza ushauri huu sawa tu na ukifanyia kazi na kuutekeleza utakupa ujiko mkubwa katikati ya mtanzuko wa kisiasa. Mwisho wa siku utajengewa senamu kwa kuwaletea taifa lao Katiba mpya.
Nakutakia kila la heri na mungu wa mbingu akubariki na akuepushe na misukosuko ya kutemeshwa ufalme wako.