Mwenyekiti wa CHASO Mwanza, Japhet Manyama apokea wito wa kufika Polisi

Mwenyekiti wa CHASO Mwanza, Japhet Manyama apokea wito wa kufika Polisi

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Mwanza, Japhet Manyama Zakayo,Leo Asubuhi amepokea wito wa kutakiwa kuripoti katika Kituo cha Polisi Nyamagana.
‎
‎Wito huo umekuja baada ya Manyama kuzungumza na vyombo vya habari kumjibu Kiliba, ambapo alimweleza Kiliba kuwekeza nguvu zake katika kupigania na kutetea maslahi ya wanafunzi kama yalivyo matakwa ya Rais wa TAHILISO, badala ya kuwa chawa wa CCM.
‎
‎Tunapinga na kukemea vikali utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kuwaita na kuwahoji vijana wa CHASO na CHADEMA kila wanapozungumzia masuala ya kisiasa, hasa pale wanapokuwa wakijibu kauli za wenzao. Inashangaza kuwa kijana wa CCM anapozungumza haitwi wala kuhojiwa, lakini kijana wa CHADEMA akizungumza tu anaitwa kwa haraka sana kuhojiwa.
‎
‎Baraza la Vijana wa Chadema,Tunawataka Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yao ya msingi kwa mujibu wa sheria na kuachana na masuala ya siasa. Polisi yeyote anayependa siasa aache kazi ya jeshi hilo na kujiunga rasmi na siasa.

Chanzo:Royal Tv

Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Mwanza, Japhet Manyama Zakayo,Leo Asubuhi amepokea wito wa kutakiwa.webp


 
Kibaya zaidi ,polisi wanajipendekeza kwa CCM .familia zao ni unga unga mwana.

Kichwani ukiwa empty ni ni aibu
 
Aliyeanzisha kuzodoa wanachadema mpaka akasema aliomba ruhusa kutukana na bi kidude kaachwa ilhali alikuja kufanya hicho alichodhamiria

Tutayapata mavuno ya hii mbegu .
 
Back
Top Bottom