Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwenyekiti wa Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Ndugu Ibrahim Musiba, leo tarehe 21 April 2025 amefanya ziara maalum katika Kata ya Masaka, Wilaya ya Iringa , ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha mahusiano na mshikamano miongoni mwa chipukizi wa chama, pamoja na kuwanoa chipukizi hao kuwa viongozi bora wa baadaye.
Ndg. Musiba amepokelewa kwa hamasa na mapokezi ya aina yake akikutana na chipukizi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo, ambapo alitoa wito kwa vijana hao kushikamana, kudumisha maadili mema, na kujifunza misingi ya uongozi unaotanguliza maslahi ya taifa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, katika kuonesha moyo wa huruma na mshikamano wa kijamii, Ndg. Musiba alishiriki katika zoezi la utoaji wa msaada wa mahitaji maalum kwa watu wenye uhitaji katika kata hiyo, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya chipukizi kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii.