Mwenyekiti wa Kijiji cha Uchira akana kutokea kifo cha Mwanafunzi wa UDOM

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kufuatia tukio la kifo cha Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma Nusura Hassan Abbdallah kuendelea kujadiliwa katika mitandao ya kijamii, vyombo vya Habari na watu mbalimbali wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika ili ukweli kupatikana, @Jambotv_ imefanya mahojiano maalumu na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Uchira Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro Julius Mkojera inapoelezwa kuwa ndipo alipofia Binti huyo,kutaka kujua ukweli wa tukio hilo.

Akiongea na JamboTV leo Mei 7.2023 Mkojera amesema kuwa tukio hilo hajaliona na halikutokea katika kijiji chake bali amekuwa akisikia uvumi huo na ameendelea kuchunguza ili kupata undani wa taarifa ya uwepo wa msiba huo bila mafanikio

"Hakuna kilichotokea katika Kijiji cha Uchira na hao watu waliotoa huo umbea naomba wakamatwe, kuna mwandishi mwingine alinipigia nikamwambia kuwa acha nichunguze nilipoanza kuchunguza kila mtu anashangaa hakuna kitu kama hicho".

"Hata leo kule Kanisani nimeuliza kuhusu hilo tukio hakuna anaye lifahamu,Hospitali ya Faraja ndio inayoweza kueleza kama walipokea mgonjwa kutoka eneo hili ila kwakweli tukio hilo halijatambulika hapa kijijini" alifafanua Mkojera.

Awali Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Kusini Bw.Meela akiongea na Jambo Tv alisema kuwa taarifa anazofahamu ni kuwa Binti huyo hakufia kwenye Kata yake.

"Baada yaa kuangalia na kuchunguza huyo Binti hakufia kwenye Kata yangu ya Kirua Vunjo Kusini" .
Jambo Tv tunaendelea kufanya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyu na tutawaletea wasomaji wetu taarifa zote kila zitakapopatikana kutoka vyanzo mbalimbali
 
Ndiyo maanani mimi nina shangaa. Inakuwaje marehemu ana ndungu lakini hadi leo hawajajitokeza hadharani kukanusha au kuthibitisha taarifa hizi. Kwani hili jambo kuna nini nyuma yake. Tangu tumeambiwa msiba mbona hatujaona au kuskia taratibu za mazishi, hivi ndugu au wazazi wake hawapo? Ebu wajitokeze waseme neno kwani kuna nini cha kuwafanya wawe mabubu juu ya mtoto wao.
 
CCM wameua elimu vyuoni,serikali za Wanafunzi zimejaa wahuni ,yaani wasomi tegemeo la jamii wamekaa kimya kukemea hao wabunge Malaya wanao haribu jamii ya watanzania lakini juzi nilisikia mbunge moja akisema wakamatwe mashoga huku walawiti,wabakaji wa Wanafunzi wakiwa bungeni
 
Vyuo dodoma ni kama madanguro

Ufuska tu ufuska

Ova
 
Ndiyo maanani mimi nina shangaa. Inakuwaje marehemu ana ndungu lakini hadi leo hawajajitokeza hadharani kukanusha au kuthibitisha taarifa hizi. Kwani hili jambo kuna nini nyuma yake. Tangu tumeambiwa msiba mbona hatujaona au kuskia taratibu za mazishi, hivi ndugu au wazazi wake hawapo? Ebu wajitokeze waseme neno kwani kuna nini cha kuwafanya wawe mabubu juu ya mtoto wao.
Ukute marehemu ni kitengo, familia kitengo, naibu waziri kutengo, bodaboda walioshuhudia ajali nao ni vitengo...hapo hauwezi ukapata taarifa yoyote ile ya maana
 
Ndiyo maanani mimi nina shangaa. Inakuwaje marehemu ana ndungu lakini hadi leo hawajajitokeza hadharani kukanusha au kuthibitisha taarifa hizi. Kwani hili jambo kuna nini nyuma yake. Tangu tumeambiwa msiba mbona hatujaona au kuskia taratibu za mazishi, hivi ndugu au wazazi wake hawapo? Ebu wajitokeze waseme neno kwani kuna nini cha kuwafanya wawe mabubu juu ya mtoto wao.
Sasa ndugu,na familia yake wanajua mtt wao kafa kwa maradhi na wanaendelea na taratibu za maziahi,nyny watu baki kinawasumbua nini ,hamtaki kuwaamini wanandugu na familia yake !!? Mambo mengine NI ajabu Sana!!
 
Yaani hii selikali yetu,kuna vitu vingine huwa inafanya tofauti sana,haioni kama inajiabisha sababu ya mjinga mmoja tu
 
Kufuatia tukio la kifo cha Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma Nusura Hassan Abbdallah kuendelea kujadiliwa katika mitandao ya kijamii, vyombo vya Habari na watu mbalimbali wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika ili ukweli kupatikana, @Jambotv_ imefanya mahojiano maalumu na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Uchira Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro Julius Mkojera inapoelezwa kuwa ndipo alipofia Binti huyo,kutaka kujua ukweli wa tukio hilo.

Akiongea na JamboTV leo Mei 7.2023 Mkojera amesema kuwa tukio hilo hajaliona na halikutokea katika kijiji chake bali amekuwa akisikia uvumi huo na ameendelea kuchunguza ili kupata undani wa taarifa ya uwepo wa msiba huo bila mafanikio

"Hakuna kilichotokea katika Kijiji cha Uchira na hao watu waliotoa huo umbea naomba wakamatwe, kuna mwandishi mwingine alinipigia nikamwambia kuwa acha nichunguze nilipoanza kuchunguza kila mtu anashangaa hakuna kitu kama hicho".

"Hata leo kule Kanisani nimeuliza kuhusu hilo tukio hakuna anaye lifahamu,Hospitali ya Faraja ndio inayoweza kueleza kama walipokea mgonjwa kutoka eneo hili ila kwakweli tukio hilo halijatambulika hapa kijijini" alifafanua Mkojera.

Awali Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Kusini Bw.Meela akiongea na Jambo Tv alisema kuwa taarifa anazofahamu ni kuwa Binti huyo hakufia kwenye Kata yake.

"Baada yaa kuangalia na kuchunguza huyo Binti hakufia kwenye Kata yangu ya Kirua Vunjo Kusini" .
Jambo Tv tunaendelea kufanya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyu na tutawaletea wasomaji wetu taarifa zote kila zitakapopatikana kutoka vyanzo mbalimbali
Umekomaa sana na hii issue. Aisee. Una moyo sana. Hongera.
 
Back
Top Bottom