Chief Kisendi Josephat Nkingwa ambaye ni Mwenyekiti wa Machifu wa Usukumani, ameyasema hayo wakati akiwa katika viunga vya Bunge ambapo aliambatana na Machifu wengine, pamoja na Mapadri kutembelea Bunge na kumuunga mkono Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kutoshiriki vikao 15 vya Bunge.
"Tumekuja kutoa taarifa Bungeni kwamba Mbunge wetu hayuko peke yake, sisi tunamuunga mkono. hata alipozungumza Bungeni kimetafutwa kipengele kidogo tu katamka neno 'Kodi' badala ya 'Tozo' basi limeshupaliwa mpaka limeonekana ni kama mtu anaangaliwa sasa kama adui.”
“Badala ya kuonekana kama ni mmoja wa wabunge ambao wanaisimamia Serikali. na Bunge kama litazembea, litakuwa linaogopa ogopa linaenda kichwa chawa hivyo, litakosa meno, litakuwa halina maana ya kwamba ni Bunge la kushauri na kuisimamia Serikali, utaishaurije Serikali kama unaisifia tangu mwanzo mpaka mwisho, kana kwamba unaongea kuhusu jopo la malaika. Hapana!”
“Ni lazima ueleze hapa pazuri tulifanikiwa hapa hatukufanikiwa, lakini ile kusifu kila kitu, kila kitu wakati kuna matatizo mengine chungu nzima mnayafunika. Kwa hoja za haraka haraka si sahihi. Bunge likikaa hivyo halina maana ya kuwepo.” - Chief Kisendi Josephat Nkingwa.